Guinea Mpya
Jump to navigation
Jump to search
Guinea Mpya ni kisiwa kikubwa katika Pasifiki upande wa kaskazini wa Australia. Ni kisiwa kikubwa cha pili duniani baada ya Greenland.
Eneo la kisiwa limegawiwa kati ya mataifa mawili:
- upande wa magharibi ni mikoa ya Indonesia ya Papua na Irian Jaya Magharibi.
- upande wa mashariki ni nchi huru ya Papua Guinea Mpya
Jiografia[hariri | hariri chanzo]
Eneo lote la kisiwa ni km² 829,200 na jumla ya wakazi ni milioni 5.2 (2004).
Kuna milima mirefu; upande wa Indonesia ni milima ya Maoke (Puncak Jaya, mita 4,884 juu ya UB) na upande wa Papua Guinea Mpya ni milima ya Bismarck (Mount Wilhelm, mita 4,509 juu ya UB).
![]() |
Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Guinea Mpya kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |