Fly (mto)
Fly ni mto mrefu wa Papua Guinea Mpya pia kwenye kisiwa cha Guinea Mpya pamoja na mto Sepik. Ina urefu wa km 1,200 na beseni lenye eneo la km² 76.000. Matawimto muhimu ya Fly ni Strickland na OK Tedi.
Mto Fly ina chanzo chake kwenye safu ya milima ya kati ya kisiwa karibu na mpaka kati ya Papua Guinea Mpya na Papua ya Indonesia. Mto unaelekea kusini na kupita tambarare kabla ya kuishia kwenye ghuba ya Papua kwa mdomo mpana sana.
Beseni la Fly lina aina nyingi sana za mimea na wanyama wa pekee ni hazina ya kiekolojia. Mtoni mwenyewe kuna aina 120 za samaki, kobe, mamba na wanyama wengine.
Mto unapitika kwa boti kwa urefu wa kilomita 1,000 kuanzia mdomo wake na kuingia ndani hivyo ni njia muhimu ya mawasiliano katika nchi yenye barabara chache.
Migodi ya dhahabu inachafua mto Fly
[hariri | hariri chanzo]Kuna matatizo mazito ya machafuko kwenye mto Fly. Migodi ya kampuni ya Ok Tedi Mining Ltd karibu na chanzo cha mto OK Tedi inateremsha mchanga mwingi pamoja na kemikali katika mto. Uchimbaji wa dhahabu na shaba hutumia kemikali za sumu kama vile zebaki na nyingine zilizosumisha maji na samaki mtoni. Kiasi kubwa cha mchanga na udongo cha tani milioni 80 chaingia mtoni kila mwaka na kuziba lalio wa mto na kusababisha mafuriko. Mafuriko ya maji yenye sumu yamesababisha kufa kwa misitu na bustani za watu kando la mto.
Kesi mbalimbali zimeendesha na kampuni imeahidi kubadilisha namna ya kuzalishwa kwa madini na kufidia watu waliopata hasara.