Nenda kwa yaliyomo

Ndege (uanahewa)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Eropleni)
Jet2
Kwa wanyama tazama makala ya Ndege (mnyama)
Boeing 767 ni mfano wa ndege kubwa inayosukumwa na injini jeti
Do 27 ni mfano wa ndege ndogo inayosukumwa na parapela. Ndege hii ilitumiwa na profesa Bernhard Grzimek kwa kuangalia wanyama katika Serengeti

Ndege (au eropleni) ni chomboanga kikubwa kinachoweza kuruka kikiwa na watu au bidhaa ndani.

Tofauti na puto au ndegeputo ni nzito kuliko hewa hivyo inahitaji chanzo cha nguvu kwa kupanda na kusafiri hewani, kwa kawaida enjini ama injini jeti au injini ya parapela pamoja na mabawa.

Ndege zinasafirisha watu na mizigo duniani kote. Ni njia ya haraka ya usafiri kushinda usafiri kama barabara, reli au meli. Ndege huhitaji uwanja wa ndege kwa kuruka au kushuka, isipokuwa aina za pekee kama helikopta zinaweza kushuka au kuruka karibu kila mahali, au ndege za bahari ama ndege za maji zinazoweza kuruka na kutua usoni kwa bahari au maziwa.

Nchi nyingi zina pia ndege za kijeshi kwa ulinzi au vita.

Kati ya makampuni makubwa yanayotengeneza ndege ni Airbus wa Ulaya na Boeing wa Marekani. Kuna makampuni mengi madogo zaidi katika nchi mbalimbali zinazotengeneza aina za ndege pia.

Ndege ya kwanza ilibuniwa na ndugu Orville na Wilbur Wright mwaka 1903. Mwanzoni ndege hazikuwa na uwezo wa kubeba abiria wengi, lakini wanasayansi wameboresha usafiri huo wa anga kwa kutengeneza ndege zenye uwezo wa kubeba abiria wengi na kwenda umbali mrefu kwa kutumia muda mfupi.

Shirika za Ndege muhimu Afrika (mwaka 2014)

Shirika Abiria
(x1000)
Idadi ya ndege Miji inayohudumiwa Chanzo Ushirikiano
1 Ethiopia Ethiopian Airlines 3.850 47 50 [1] Star Alliance
2 Afrika Kusini South African Airways 3.800 67 60 [2] Star Alliance
3 Kenya Kenya Airways 2.010 19 55 [3] Sky Team
4 Uganda Africa Safari Air 1.700 12 10 Sky Team

Marejeo

  1. [1]
  2. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-03-06. Iliwekwa mnamo 2014-01-18. {{cite web}}: Unknown parameter |= ignored (help)
  3. "www.skyteam.com". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-08-16. Iliwekwa mnamo 2013-01-01.
Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ndege (uanahewa) kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.