Ndege (uanahewa)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Boeing 767 ni mfano wa ndege kubwa inayosukumwa na injini jeti
Do 27 ni mfano wa ndege ndogo inayosukumwa na parapela. Ndege hii ilitumiwa na profesa Bernhard Grzimek kwa kuangalia wanyama katika Serengeti
Kwa wanyama tazama makala ya Ndege (mnyama)

Ndege (au eropleni) ni chomboanga kikubwa kinachoweza kuruka wakati kikiwa na watu au bidhaa ndani. Tofauti na puto au ndegeputo ni nzito kuliko hewa hivyo inahitaji chanzo cha nguvu kwa kupanda na kutembea hewani, kwa kawaida enjini ama injini jeti au injini ya parapela pamoja na mabawa.

Ndege zasafirisha watu na mizigo duniani. Ni njia ya haraka ya usafiri duniani kushinda usafiri kawa barabara, reli au meli. Ndege huhitaji uwanja wa ndege kwa kuruka au kushuka isipokuwa aina za pekee kama helikopta zinaweza kushuka au kuruka karibu kila mahali.

Nchi nyingi zina pia ndege za kijeshi kwa ulinzi.

Kati ya makampuni makubwa yanayotengeneza ndege ni Airbus wa Ulaya na Boeing wa Marekani. Kuna makampuni mengi madogo zaidi katika nchi mbalimbali zinazotengeneza aina za ndege pia.

Shirika za Ndege muhimu Afrika(Mwaka 2014)

Shirika Abiria
(x1000)
Idadi ya ndege Miji inayohudumiwa Chanzo Ushirikiano
1 Ethiopia Ethiopian Airlines 3.850 47 50 [1] Star Alliance
2 Afrika Kusini South African Airways 3.800 67 60 [2] Star Alliance
3 Kenya Kenya Airways 2.010 19 55 [3] Sky Team
4 Uganda Africa Safari Air 1.700 12 10 [4] Sky Team

Marejeo

  1. [1]
  2. [2]
  3. www.skyteam.com
  4. Safari Air.jsp www.skyteam.com
ThreeCoins.svg Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ndege (uanahewa) kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.