Uholanzi
|
|||||
| Hadabu ya Taifa: Je maintiendrai (Kifaransa) kwa Kiswahili, Nitastahimili |
|||||
| Lugha za Taifa |
Kiholanzi kwa mkoa wa Friesland: Kifrisi |
||||
| Mji Mkuu | Amsterdam | ||||
| Makao ya Serikali | Den Haag | ||||
| Mfalme | Koning Willem-Alexander | ||||
| Waziri Mkuu | Mark Rutte | ||||
| Eneo - Jumla - % Maji |
41,526 km² 18.41 |
||||
| Umma - Jumla - msongamano |
16,856,620 (Julai 2014) 406.4/km² |
||||
| GDP - Jumla - kwa kipimo cha umma |
$625 bilioni $ 30,500 |
||||
| Uhuru - Tangazwa - Kukubaliwa |
Kutoka Hispania 26 Julai 1581 30 Januari 1648 |
||||
| Fedha | Euro € EUR | ||||
| Saa za Eneo | UTC +1 | ||||
| Wimbo wa Taifa | Wilhelmus | ||||
| TLD mtandao | .nl | ||||
| Kodi ya simu | 31 | ||||
Uholanzi ni nchi ya Ulaya ya Magharibi. Imepakana na Ujerumani upande wa mashariki, Ubelgiji upande wa kusini na Bahari ya Kaskazini (North Sea) upande wa magharibi na kaskazini.
Uholanzi ni sehemu ya "Ufalme wa Nchi za Chini" (Kingdom of the Netherlands) pamoja na visiwa vya Aruba, Curaçao na Sint Maarten, mbali ya visiwa vingine vitatu vya Karibi vya Uholanzi.
Jina la Uholanzi limetokana na “Holland”, eneo la magharibi la nchi hii. Watu wengi hutumia jina hilo, lakini wakazi wenyewe wanaiita nchi yao “Nederland” inayomaanisha "nchi ya chini". Kwa kweli, sehemu kubwa ya Uholanzi iko chini ya usawa wa bahari. Waholanzi wamejenga maboma kuzuia maji yasienee yakifurika.
Yaliyomo
Jiografia[hariri | hariri chanzo]
Akifika Uholanzi kwa uwanja wa ndege wa Schiphol, msafiri anastaajabu nchi ilivyo tambarare. Kwa kweli, kuna sehemu zenye vilima, lakini sehemu kubwa zaidi ya Uholanzi ni tambarare.
Mahali pa juu kabisa nchini ni Kilima cha Vaals, upande wa kusini wa mkoa wa Limburg, kwa 322 m. Mahali pa chini kabisa ni karibu na Nieuwerkerk aan de IJssel, mkoa wa Zuid Holland, kwa -6.76 m (mita 6.76 chini ya usawa wa wastani wa bahari).
Vipande vikubwa vya nchi vimepatikana kutoka ziwa au bahari. Ili kufanya hivyo boma linajengwa kuzunguka ziwa au sehemu ya bahari, kisha maji yanavutwa kwa bomba. Mahali kati ya boma huitwa “polder”. Mkoa mmoja mzima, Flevoland, umepatwa kwa maji ya “Zuiderzee” (Bahari ya Kusini). Kwa sababu hiyo watu husema: “Mungu aliumba dunia lakini Waholanzi waliumba Uholanzi.” Hata sasa sehemu muhimu ya Uholanzi ni maji: 18%.
Maboma mengine makubwa yamejengwa upande wa kusini magharibi wa nchi ili ya kuzuia maji yasienee mikoa ya Zeeland na Zuid Holland. Mradi huu huitwa “Deltawerken” au Ujenzi wa Delta. “Oosterscheldekering” au boma la mto wa Oosterschelde ni jengo linaloshangaza. Urefu wake ni 9 km na katikati yake kuna malango makubwa 62 ambayo hujifunga wenyewe kila wakati ambapo maji ya bahari yakifura zaidi ya 3 m. Barabara kuu inapitia juu ya boma hili.
Mito[hariri | hariri chanzo]
Mito mikubwa kadhaa inaingia Uholanzi na kutiririka katika Bahari ya Kaskazini. Mto Rijn (Mto Rhine) unaingia kwa Tolkamer upande wa mashiriki, na karibu na Nijmegen Mto Waal unajitenga ambao unachukua 70% ya maji. Mto IJssel unajitenga karibu na Westervoort na kwenda upande wa kaskazini. Mto Maas (Mto Meuse) unaingia Uholanzi upande wa kusini wa Limburg, na karibu na Mook unageuka upande wa magharibi. Mto Schelde unaingia upande wa kusini wa Zeeland.
Mikoa[hariri | hariri chanzo]
Uholanzi umegawanyika katika mikoa 12. Kila mkoa unatawaliwa na gavana ambaye huitwa “Commissaris van de Koningin” isipokuwa yule wa Limburg ambaye huitwa “Gouverneur”. Mikoa na miji mikuu yao ni :
| Mkoa | Mji mkuu |
|---|---|
| Groningen | Groningen |
| Friesland | Leeuwarden |
| Drenthe | Assen |
| Overijssel | Zwolle |
| Gelderland | Arnhem |
| Utrecht | Utrecht |
| Flevoland | Lelystad |
| Noord-Holland | Haarlem |
| Zuid-Holland | Den Haag (The Hague) |
| Zeeland | Middelburg |
| Noord-Brabant | ’s-Hertogenbosch (Den Bosch) |
| Limburg | Maastricht |
Miji mikubwa[hariri | hariri chanzo]
| Mji | Wakazi |
|---|---|
| Amsterdam | 742,011 |
| Rotterdam | 600,000 |
| Den Haag | 476,000 |
| Utrecht | 281,569 |
| Eindhoven | 209,399 |
Trafiki[hariri | hariri chanzo]
Katika Uholanzi barabara daima zina msongamano wa magari. Hii ni kwa sababu watu wanakwenda kazini asubuhi hadi kurejea jioni, na wanaoishi Uholanzi ni wengi, na kufanya kazi nyingi sana.
Watu[hariri | hariri chanzo]
Wakazi wengi wana asili ya makabila ya Kijerumani, lakini kuna wahamiaji wengi pia. Lugha ya kawaida ni Kiholanzi.
Upande wa dini, 39% ni Wakristo, hasa Wakatoliki (24.6%) na Wakalvini (10.8%). 5.8% ni Waislamu, 1.4% Mabanyani na 1.2% Wabuddha.
Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]
Historia, jiografia na siasa[hariri | hariri chanzo]
- Overheid.nl - Lango rasmi la serikali ya Uholanzi
- Ramani na takwimu
- Mikoa ya Uholanzi
- CBS - Takwimu rasmi
- Makala ya Encarta kuhusu Uholanzi
- Government.nl - Tovuti rasmi ya serikali ya Uholanzi
- CIA - The World Factbook -- Netherlands
- Habari za Uholanzi: Radio Netherlands - Redio ya Uholanzi kwa lugha ya Kiingereza
Kusafiri[hariri | hariri chanzo]
Netherlands travel guide kutoka Wikisafiri- World66's guide to the Netherlands - Kiongozi cha kusafiri kinachoandikwa na watumiaji.
- Kiongozi cha kusafiri katika Uholanzi
- Picha za Uholanzi
- Just Landed Netherlands - Habari za manufaa kwa kuhamia Uholanzi
Viungo anuwai[hariri | hariri chanzo]
- Ujenzi wa Delta kwa mtandao
- Keukenhof Bustani za Maua - Picha nzuri mno za bustani za maua katika Uholanzi.
- Familia ya kifalme ya Uholanzi
- Kiholanzi kwa wasemao Kiingereza
- Orodha ya majengo marefu 1500 katika Uholanzi
| Nchi za Umoja wa Ulaya | |
|---|---|
| Austria | Bulgaria | Denmark | Estonia | Hispania | Hungaria | Ireland | Italia | Kroatia | Kupro | Latvia | Lituania | Luxemburg | Malta | Poland | Slovakia | Slovenia | Romania | Ubelgiji | Ucheki | Ufalme wa Muungano | Ufaransa | Ufini | Ugiriki | Uholanzi | Ujerumani | Ureno | Uswidi | |
|
||||||||||||||
| Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Uholanzi kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |