Pasifiki

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Bahari ya Pasifiki duniani

Pasifiki ni bahari kubwa kuliko bahari zote duniani.

Pasifiki iko kati ya Bara la Amerika kwa upande wa mashariki na Bara la Asia / Australia upanda wa magharibi. Eneo lake ni karibu nusu ya uso wa dunia. Eneo lake ni kilometa za mraba milioni 179.7 ambayo si bahari kubwa tu bali pia ni eneo kubwa kuliko nchi kavu yote duniani. Visiwa vyake vingi huhesabiwa mara nyingi pamoja na Australia kama "Australia na Pasifiki".

Pasifiki ina kina cha wastani wa mita 4,028; kina kikubwa katika mfereji wa Mariana kinafikia mita 11,034.

Pasifi inayoonekana kutoka angani; Australia iko upande wa kushoto chini

Kuna visiwa zaidi ya 25,000 katika Pasifiki vingi ni vidogo sana.

Bahari za pembeni ziko hasa upande wa Asia / Australia. Kati ya hizo ni: Bahari ya Calebes, Bahari ya Uchina ya Kusini, na Bahari ya Mashariki.

Jina la Pasifiki (Kilatini: yenye amani, yaani kimya) limetokana na Wazungu wa kwanza waliovuka bahari hii mwaka 1520 BK kutoka Amerika ya Kusini hadi Ufilipino wakaikuta kuwa ni bahari tulivu. Lakini Pasifiki inaweza kuwa na dhoruba kali sana. Ni eneo lenye matetemeko ya ardhi mengi yanayosababisha mawimbi haribifu ya tsunami ambayo yalimaliza miji na vijiji ufukoni.

Sciences de la terre.svg Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Pasifiki kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.