Kura
Mandhari
Kwa maana nyingine, tazama Kura (bahati).
Kwa maana nyingine, tazama Mto Kura.
Kura ni tendo au njia ya kawaida kwa kundi la watu ama kuchagua kiongozi wanayemtaka ama kuchukua maamuzi wanayoona yanafaa.
Taratibu za kupiga kura zinaweza kuwa mbalimbali, kwa mfano kuhusu nani apige, nani apigwe kura, kwa namna gani n.k.: mara nyingi ni muhimu itunzwe siri kuhusu kura iliyotolewa na kila mtu, aweze kuitoa bila hofu au shuruti kutoka nje.
Demokrasia inapenda chaguzi zifanyike na maamuzi mengi yachukuliwe baada ya mjadala mpana na kura za wengi.
Pengine kupiga kura ni wajibu unaosisitizwa na sheria, lakini mara nyingi zaidi mwenye haki ya kupiga kura anaweza kuachiwa hiari asiitumie, tena dini ndogo chache zinakataza waumini wasipige kura kamwe.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]Wikimedia Commons ina media kuhusu:
- A history of voting in the United States from the Smithsonian Institution.
- A New Nation Votes: American Elections Returns 1787-1825 Ilihifadhiwa 25 Julai 2008 kwenye Wayback Machine.
- Can I Vote?—a nonpartisan US resource for registering to vote and finding your polling place from the National Association of Secretaries of State.
- The Canadian Museum of Civilization — A History of the Vote in Canada
Makala hii kuhusu mambo ya sheria bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kura kama historia yake au uhusiano wake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |