Siri

Siri (kutoka neno la Kiarabu) ni jambo lolote ambalo mtu analiona haifai kumshirikisha mtu yeyote yule, haijalishi ni nani.
Kila mmoja ana haki ya kuwa na siri zake.
Katika maisha ya jamii, siri ni muhimu, kiasi kwamba ni wajibu kwa baadhi ya kazi, kama vile ushauri, uganga, huduma za benki n.k.
Siri kali zaidi, katika Kanisa Katoliki, ni ile ya padri kuhusu maungamo aliyopokea katika sakramenti ya kitubio.
Makala bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |