Upadri

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Padri)
Jump to navigation Jump to search

Upadri ni daraja takatifu ya kati ya uongozi wa Kanisa Katoliki na madhehebu mengine kadhaa.

Unatolewa na Askofu kwa kumwekea mtu mikono kichwani na kumuombea ili atoe huduma za kikuhani, hasa kwa kuhubiri rasmi Neno la Mungu, kuadhimisha Ekaristi na sakramenti nyingine na kuongoza jumuia za waamini.

Upadri unatolewa kwa namna ya kudumu, usiweze kurudiwa wala kufutwa.

Shirika la kwanza la Kanisa la Kikristo katika Yerusalemu lilikuwa na wasomi wengi sawa na lile la sinagogi la Uyahudi, lakini lilikuwa na Halmashauri au chuo cha wazee waliowekwa (πρεσβύτεροι, wazee )

Katika Matendo ya Mitume 11:30 na 15: 22 tunaona mfumo wa washirika wa uongozi huko Yerusalemu ingawa unaongozwa na Yakobo Mdogo, askofu wa kwanza wa mji. Katika Matendo 14: 23, Mtume Paulo anaweka wakubwa katika makanisa aliyoanzisha.

Christianity Symbol.png Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Upadri kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.