Wimbo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

Wimbo/nyimbo ni tungo zenye kufuata mapigo fulani ya kimi za kiafuziki yenye mahadhi ya kupanda na kushuka kwa mawimbi ya sauti (urari wa sauti) na mpangilio maalumu wa maneno.

Nyimbo huundwa kwa lugha ya mkato na matumizi ya lugha ya picha (taswira).

Muundo wa nyimbo huwa ni kuimbika na mizani ya kila mstari mara nyingi huwa inalingana.

Nyimbo aghalabu huambatana na ala za muziki kama vile ngoma, zeze, marimba, makofi, vigelegele na kadhalika.

Wahusika wa nyimbo huwa ni mtu mmoja au kikundi cha watu. Mashairi ya nyimbo huimbwa popote pale panapostahili kulingana na tukio au muktadha unaofungamana na wimbo. Hivyo basi kuna nyimbo za dini, harusi, siasa, jando/unyago, kilimo, nyimbo za kuwinda na kadhalika.

Musical notes.svg Makala hii kuhusu mambo ya muziki bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Wimbo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.