Michezo ya watoto
Michezo ya watoto ni michezo mbalimbali inayochezwa na watoto. Mara nyingi michezo hiyo huigiza maisha halisi ya jamii. Watoto hucheza kutokana na tamaduni zao, kwa mfano kama utamaduni wa eneo hilo ni ngoma basi mara nyingi watoto watacheza na kupiga ngoma licha ya kuchanganya na michezo mingine.
Michezo ya watoto huwasaidia kukua kiakili na kimwili pia. Ni muhimu watoto waweze kushiriki michezo mbalimbali kwa madhumuni ya kuwajenga.
Michezo ya watoto ipo ya aina mbalimbali, kwa mfano Afrika Mashariki kuna:
- Bembea
- Buye
- Esta
- Joka
- Kibereko
- Kinyulinyuli
- Kioo
- Kombolela (butuo)
- Kukimbia kwa miguu mitatu
- Kukimbia na chupa kichwani
- Kukimbia na kijiko
- Kukimbiza kuku
- Kula mbakishie baba
- Kuruka
- Kuruka kamba
- Kuruka viunzi
- Kuvuta kamba
- Maigizo dhima
- Mdako
- Nage
- Rede
- Saga koboa
- Tikri
- Tobo
- Ukuti ukuti
- Ulingo bayoyo
- Visoda
- Wino
na kadhalika.
Umuhimu
[hariri | hariri chanzo]- Kuimarisha afya za watoto
- Kujenga uwezo wa kufikiri
- Kujenga umoja na mshikamano katika jamii
- Kustawisha utamaduni wa jamii husika.
Hasara
[hariri | hariri chanzo]- Kuigana tabia mbaya miongoni mwao
- Kuambukizana maradhi
- Kuumizana
- Uharibifu wa mali za jamii.
Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Michezo ya watoto kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |