Wino (mchezo)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Wino ni mchezo asilia wa watoto wa Afrika Mashariki.

Mchezo huu unashirikisha watoto watatu na kuendelea. Vifaa vinavyotumika ni chupa na mchanga ambao hukusanywa kwa wingi hadi kutengeneza kama mlima. Chupa huwekwa juu ya mlima huo.

Wachezaji wawili husimama mbali na mchanga ambao huwa katikati pamoja na mchezeshaji mmoja. Huyo anatakiwa kujaza mchanga ndani ya chupa bila kupigwa na wenzake kwa mpira; kwa ajili hiyo anaukwepa au akiudaka anaurusha mbali apate muda zaidi. Akifaulu amefunga goli.

Blank template.svg Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Wino (mchezo) kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.