Mtoto

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Watoto)
Watoto nchini Namibia.
Ramani ya dunia inayoonyesha idadi ya watu wenye umri wa chini ya miaka 15 mwaka 2005.

Mtoto ni mwanadamu mwenye umri mdogo, asiye mtu mzima bado. Kuna tofauti katika tamaduni mbalimbali kuhusu umri ambapo mtu si mtoto tena.

Mara nyingi miaka kabla ya kubalehe inatazamiwa kuwa kipindi cha utoto na baadaye mtu anaitwa kijana.

Sheria[hariri | hariri chanzo]

Umoja wa Mataifa umetoa azimio juu ya haki za watoto (Convention on the Rights of the Child) lililokubaliwa na karibu nchi zote za dunia isipokuwa Marekani na Somalia kuwa mkataba wa kimataifa. Mkataba huu unaeleza ya kwamba utoto ni kipindi hadi kufikia umri wa miaka 18.

Mkataba wa Kiafrika juu ya haki na ustawi wa watoto (African Charter on the Rights and Welfare of the Child) uliokubaliwa na Umoja wa Afrika unamwona pia kila mtu hadi umri wa miaka 18 kuwa mtoto.

Kuna nchi zinazotofautiana kisheria kati ya watoto na vijana. Kwa mfano Ujerumani inawaangalia wale walio kati ya miaka 14 na 18 kuwa vijana na kuwapa haki tofauti na watoto na watu wazima.

Mtoto kwaujumla hapewi madaraka kama mtu mzima, yuko chini ya usimamizi na uangalizi wa wazazi au walezi.

Utamaduni[hariri | hariri chanzo]

Hali ya mtoto inaamuliwa zaidi na utamaduni na mapokeo yake. Kuna tamaduni ambako kijana wa miaka 16 anatazamwa kuwa mtu mzima tayari. Hasa wasichana wanaolewa mapema na baadaye wanatazamwa kuwa mwanamke na mama kamili hata wakiwa na umri mdogo tu.

Katika mazingira ya wakulima au wafugaji mtoto anategemewa kufanya kazi kulingana na nguvu zake; anaweza kupewa wajibu kamili hata kama kisheria anatazamwa kuwa mtoto bado.

Kwa lugha mbalimbali katika uhusiano na wazazi wake mtu anaendelea kuitwa mtoto hata kama ameshakuwa mtu mzima na ameshazaa mwenyewe.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mtoto kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.