Nenda kwa yaliyomo

Umoja wa Afrika

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Umoja wa Afrika
Majina mengine tano rasmi[1]
Wimbo:
"Hebu wote kuungana na kusherehekea pamoja"
     Nchi wanachama      Nchi zilizosimamishwa
Miji mikuuAddis Ababa (serikali)
Johannesburg (bunge)
Mji mkubwaLagos
AinaShirika la kimataifa
 • Mwenyekiti
João Lourenço
 • Mwenyekiti wa Tume
Moussa Faki
 • Rais wa Bunge
Fortune Z. Charumbira
WanachamaNchi 55
Uanzishaji
25 Mei 1963
 • Umoja wa Afrika
9 Julai 2002
Idadi ya watu
 • Kadirio la 20241,515,140,849[2]
PLT (PPP)Kadirio la 2022
 • Jumla $9.0 Trilioni
 • Kwa kila mtu $8,600
PLT (Kawaida)Kadirio la 2022
 • Jumla $3.1 Trilioni
 • Kwa kila mtu$2,980
HDI (2022) 0.558 kati
Gini (2022)41.5
Tovuti rasmi:
https://au.int/sw

Umoja wa Afrika (UA) ni muungano wa bara unaojumuisha nchi wanachama 55 zilizo katika bara la Afrika. Ulianzishwa tarehe 26 Mei 2001 huko Addis Ababa, Ethiopia, na kuzinduliwa rasmi tarehe 9 Julai 2002 mjini Durban, Afrika Kusini, ukichukua nafasi ya Jumuiya ya Umoja wa Afrika (OAU). Mji mkuu wa UA ni Addis Ababa.


Umoja huu unaendeleza kazi za Umoja wa Muungano wa Afrika (kwa Kiingereza: Organisation of African Union - OAU) uliokuwepo 1963 hadi 2002.

Nia ya umoja huu ni kujenga muundo na mfumo wa kisiasa, wa kiuchumi, na wa kijamii ili kufikia wakati ambapo bara la Afrika litakuwa na bunge moja, benki moja, jeshi moja, raisi mmoja, sarafu moja, n.k.

Dhumuni kubwa la umoja huu ni kuunganisha nguvu za mataifa ya Afrika ili kuweza kutatua matatizo yanayokabili bara hili kama vile vita, njaa, Ukimwi, n.k.

Nchi wanachama

Umoja wa Afrika ina nchi wanachama 55, yaani nchi zote za bara la Afrika (baada ya kurudi kwa Moroko, iliyokuwa imejiondoa mwaka 1985 kwa sababu UA ilitambua Sahara ya Magharibi kuwa nchi huru wakati Moroko inadai ni eneo la majimbo yake ya kusini). [3][4][5]

Mkutano wa kwanza wa Bunge la Umoja wa Afrika ulifanyika mwaka 2004 huko Afrika Kusini.

Mikutano mikuu ya UA

  1. Durban (Afrika Kusini): 9-11 Julai 2002.
  2. Maputo (Msumbiji): 10-11 Julai 2003.
  3. Sirte (Libya), mkutano wa dharura: Februari 2004.
  4. Addis Ababa (Ethiopia): 6-8 Julai 2004.
  5. Abuja (Nigeria): 24-31 Januari 2005.
  6. Sirte (Libya): 28 Jun. - 5 Julai 2005.
  7. Khartoum (Sudan): 16-24 Januari 2006.

Viongozi

Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya UA ni N. Dlamini-Zuma.

Spika wa Bunge la Umoja wa Afrika ni Roger Nkodo Dang.

Marejeo

  1. "Official Languages AU "Art. 11 AU" Protocol on amendments to the constitutive act of the African Union" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2014-06-30. Iliwekwa mnamo 2014-09-06.
  2. worldometers. "Idadi ya Watu, Afrika" (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2025-02-15.
  3. [1]
  4. "Mbona Morocco si mwanachama wa Umoja wa Afrika?". BBC. 15 Julai 2016.
  5. "Morocco yarudi katika Umoja wa Afrika AU". BBC. 31 Januari 2017.

Viungo vya nje