Biashara ya ng'ambo ya Sahara

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Oasisi ya Bilma mjini kaskazinimashariki mwa Niger, kukiwa na mharara wa Kaouar kwa nyuma

Biashara ya ng'ambo ya Sahara (vilevile Biashara ya Masafa Marefu ya Afrika ya Magharibi) ilikuwa biashara iliyohusisha Afrika ya Magharibi na Afrika ya Kaskazini kupitia jangwa la Sahara.

Biashara hiyo ni mfano mzuri wa biashara za kanda au masafa marefu ambayo yaliongozwa katika upande wa Afrika Magharibi.

Biashara hiyo ilianza mnamo karne ya 4 na iliendelea zaidi hadi katika karne ya 17 ambapo ilianguka mazima.

Biashara ilikuwa na matokeo kadha wa kadha katika historia ya Afrika Magharibi na ya Afrika kwa ujumla.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Washiriki[hariri | hariri chanzo]

Washirika wakubwa wa biashara hii walikuwa watu kutoka Mataifa ya Kimagharibi ya Sudani, Ghana, Mali na Songhai na baadhi ya watu kutoka mjini Kaskazini mwa Afrika.

Kutoka Afrika Magharibi[hariri | hariri chanzo]

Ilihusisha kikundi cha Wasoninke, Wamandika, Wayoruba, Wafulani, Wahausa na wengineo wengi.

Kutoka Afrika Kaskazini[hariri | hariri chanzo]

Ilihusisha kikundi cha Waarabu, Waberberi, Watuareki na wengine wengi.

Bidhaa au vitu vilivyokuwa vinauzwa[hariri | hariri chanzo]

Bidhaa zilizokuwa zinauzwa ni mchanganyiko, lakini vilevile mauzo yaliendana na kanda. Mifano:

Kutoka Afrika Magharibi[hariri | hariri chanzo]

Kutoka ndanindani kabisa ya misitu ya Afrika Magharibi, bidhaa zilikuwa dhahabu, fedha, ngozi za wanyama, pembe za ndovu, nta ya nyuki, asali and vitu vingine vya thamani vilivyoweza kubebwa.

Kutoka Afrika Kaskazini[hariri | hariri chanzo]

Kutoka Kaskazini, Waberberi na Waarabu walileta bidhaa ndogondogo kwa mfano shanga, miwani, silaha na vingine vingi. Kwa upande wa jangwa la Sahara chumvi ilikuwa inapatikana kutoka Taghaza, Fez na Bilima. Aina kuu za usafiri wakati wa biashara hii ilikuwa punda, farasi na wakati mwingine walitembea kwa miguu. Lakini baadaye katika karne ya 7, ngamia waliletwa na Waarabu ambao waliwasili wakitokea Mashariki ya Kati na kuanza kutumika kama chombo kikuu cha usafiri kupitia Sahara.

Muundo wa biashara[hariri | hariri chanzo]

Biashara ilipangwa kwa mtindo wa misafara kama msururu ambayo ilianza kutoka kila upande wa Magharibi na Kaskazini mwa Afrika kupitia jangwa la Sahara. Misafara hiyo ilikuwa kama ifuatavyo:

(a) Msafara wa Magharibi[hariri | hariri chanzo]

Msafara ulianza kutoka Sijilmasa na Fez huko nchini Morocco. Halafu ukapitia Taghaza, Taoden, Watala, Audaghost, Kumbi Saleh hadi Timbuktu.

(b) Msafara wa Kati[hariri | hariri chanzo]

Msafara ulianza kutoka Tunis wakapitia Ghat, Kano kisha ukaenda zake na kupitia jangwani hadi Gao na mwisho kabisa Hausa.

(c) Msafara wa Mashariki[hariri | hariri chanzo]

Msafara huu ulianzia mjini Tripoli ukaenda zake hadi Marzul na mwisho kabisa ukamalizikia mjini Bilima.

Sababu zilizopelekea kukua kwa biashara[hariri | hariri chanzo]

Msafara wa ngamia wa siku hizi karibu na Milima ya Ahaggar katikati ya jangwa la Sahara, 2006.

Ukuaji na uendeleaji wa Biashara ya Ng'ambo ya Sahara iliathiriwa na mambo kadha wa kadha. Miongoni mwa sababu hizo ni:

A) Siasa Imara

Katika nchi za Magharibi na Kaskazii hali ilikuwa shwari kabisa, hakukuwa na vita wala nini. Hili lilitoa chumba cha ukuaji wa biashara ya ng'ambo.

B) Eneo la Kijiografia

Mahali penyewe panawezesha maendeleo ya kibiashara. Hili lilitokana na ukweli ni kwamba Magharibi na Kaskazini mwa Afrika zimepakana mno kupitia jangwa la Sahara.

C) Upatikanaji wa bidhaa

Upatikanaji wa bidhaa huko Magharibi na Kaskazini mwa Afrika kulipelekea kukua kwa biashara ya ng'ambo.

D) Utambulishaji wa ngamia kama zana ya kusarishia

Ngamia alitambulishwa na Waarabu kama zana kuu ya kusafirishia kupitia jangwa la Sahara katika karne ya 7. Hili lilirahisha shughuli za usafirishaji kupitia jangwani hivyo basi kupelekea ongezeko la ukuaji wa biashara hii.

E) Uwepo wa chemchemi jangwani

Haya ni maeneo ya jangwa yenye vyanzo vya maji. Uwepo wa maeneo haya yenye maji umepelekea upatikanaji wa maji hayo kwa ajili ya ngamia na wafanyabiashara, hivyo kuzidi kuchochea maendeleo ya ukuaji wa kibiashara.

F) Ujio wa Waarabu

Ujio wa Waarabu katika Afrika ya Kaskazini hasa kwenye karne ya 7 kulipelekea upatikanaji wa bidhaa mpya kama vile vitu vya chakula, mavazi, ngamia, bunduki na unga wa bunduki. Katika njiapanda hii, ukuaji wa biashara ukawa hauepukiki tena.

G) Uongozi mzuri wa falme

Karibia falme zote hasa huko Afrika Magharibi zilikuwa na viongozi wazuri waliokuwa wanatoa hamasa ya ukuaji wa biashara. Falme kama ya Ghana na Mali zilitoa mpangilio mzuri wa biashara.

Sababu zilizopelekea kuanguka kwa biashara[hariri | hariri chanzo]

Mwishoni mwa karne ya 14, idadi ya misafara ya biashara ikaanza kuanguka. Zifuatazo zilikuwa sababu kuu zilizopelekea kuanguka kwa biashara ya ng'ambo:

A) Pepo kali za jangwani

Wafanyabiashara wengi walitelekeza biashara zao kwa kufuatia upepo mkali uliokuwa unavuma jangwani. Pepo hizi zilifanya ugumu sana wa ukuaji na uendelezaji wa biashara.

B) Uvamizi wa Walmoravidi

Hawa walikuwa Waarabu wa kutoka Mashariki ya Kati, wakataka kueneza Uislamu mjini Kaskazini na Magharibi mwa Afrika kwa mabavu. Hili nalo lilipelekea kudhoofisha biashara.

C) Vita vitakatifu

Hivi vilikuwa vita baina ya Waislamu na hao wasiotaka kufuata dini na utamaduni wa Kiislamu, hasa upande wa Afrika ya Magharibi. Matokeo yake, Vita vitakatifu hivi vimefanya ugumu wa uwepo wa amani na utulivu ndani ya misafara ya biashara na hivyo basi biashara ikaanguka.

D) Ujio wa Wazungu

Ujio wa Wazungu upande wa Kaskazini na Magharibi mwa Afrika kulipelekea muendelezo wa migogoro kwa vile Wazungu nao walitaka kueneza Ukristo na kushikilia biashara zote za misafara hii. Hili nalo lilichangia mazima katika kubomoa biashara.

E) Kuanguka kwa falme

Kuanguka kwa baadhi ya falme, kama vile Ghana na Mali, nako kulichangia kudidimia kwa biashara kutokana na ukweli wa kwamba falme hizi zilitoa mwongozo wa kibiashara kupitia viongozi wao ambao walikuwa wanawasimamia wafanyabiashara.

F) Kuibuka kwa Biashara ya utumwa kupitia Atlantiki

Kuibuka kwa biashara ya pembetatu mwishoni mwa karne ya 15 kulichangia kuanguka mazima kwa biashara ya ng'ambo ya Sahara ambapo biashara ilihamia huko Amerika na Ulaya.

Matokeo ya biashara ya ng'ambo ya Sahara[hariri | hariri chanzo]

Biashara ya ng'ambo ya Sahara ilikuwa na matokeo (madhara) kadha wa kadha kwa Afrika Magharibi na Kaskazini kwa ujumla. Baadhi ya matokeo hayo ni haya:

(i)Utambulisho wa tamaduni mpya[hariri | hariri chanzo]

Biashara ilileta tamaduni mpya kwa Afrika Magharibi na Kaskazini. Miongoni mwa tamaduni hizo ni mtindo wa mavazi, vyakula, lugha na vingine vingi vilivyoingia katika ukanda huu.

(ii)Ongezeko la watu[hariri | hariri chanzo]

Biashara pia ilipelekea kuongezeka kwa watu katika Afrika Magharibi na Kaskazini hasa kwa ujio wa Waarabu na watu wengine kutoka sehemu mbalimbali.

(iii)Ukuaji wa miji na vijiji[hariri | hariri chanzo]

Biashara ya Ng'ambo ilichangia kwa kiasi kikubwa katika maendeleo ya miji na vijiji katika Afrika Magharibi na Kaskazini - kama vile Timbuktu, Mandika, Kumbi Saleh, Taghaza, Tripoli na mingine mingi.

(iv)Uenezi wa dini ya Kiislamu[hariri | hariri chanzo]

Biashara pia ilipelekea kuenea kwa dini ya Kiislamu kwa Afrika Magharibi na Kaskazini kwa ujumla - ambapo baadhi ya Waafrika walitelekeza dini zao za jadi na kujiunga na Uislamu.

(v)Ndoa mseto[hariri | hariri chanzo]

Ndoa za mseto zilitokea baina ya Waafrika kutoka Magharibi na hao kutoka Kaskazini kwa kufuatia biashara hii. Vilevile ndoa za mseto zilitokea baina ya Waarabu na Waafrika.

(vi)Ukuaji wa falme/madola[hariri | hariri chanzo]

Biashara pia ilipelekea kukua kwa falme nyingi huko Kaskazini na Magharibi mwa Afrika. Baadhi ya madola na falme hizo ni Ghana na Mali.

(vii)Kuibuka kwa viongozi na wafanyabiashara wakubwa[hariri | hariri chanzo]

Biashara ya ng'ambo ilipelekea kuibuka kwa viongozi wenye nguvu (athira/ushawishi) mkubwa hasa upande wa Magharibi. Viongozi hao ni pamoja na Sundiata Keita, Mansa Mussa, Askia Muhammad na Sunni Ali.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Jisomee[hariri | hariri chanzo]