Dhahabu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta


Dhahabu (Aurum)
Au-TableImage.png
Jina la Elementi Dhahabu (Aurum)
Alama Au
Namba atomia 79
Uzani atomia 106,42 u
Valensi 2, 8, 18, 32, 18, 1
Kiwango cha kuyeyuka 1337,33 K (1064,18 °C)
Kiwango cha kuchemka 3129 K (2856 °C)


Punje za dhahabu jinsi zinavyopatikana kwenye ardhi au mtoni

Dhahabu (kutoka kar. ذهب dhahab; pia: auri kutoka Kilatini aurum kama jina la kisayansi) ni elementi yenye namba atomia 79 katika mfumo radidia na uzani atomia ni 196.966569. Alama yake ni Au.

Ni metali adili nzito yenye rangi ya njano nyeupe hadi njano nyekundu. Kiwango chake cha kuyeyuka ni 1337,33 K (1064,18 °C). Dhahabu haiathiriwa kikemia hi ni sababu ya kungaa kwa miaka mingi kwa sababu haishikwi na kutu.

Ni kati ya metali za kwanza zilizotumiwa na wanadamu. Sababu yake ni ya kwamba dhahabu hutokea kama metali tupu (kwa kawaida si kama sehemu ya mchanganyiko wa madini inapohitaji kuondolewa kwanza), halafu rangi yake ya kuvutia na tabia yake ya kuchongeka baridi kwa kuponda tu kuwa bati au waya. Ni metali laini haifai kwa silaha au vifaa vya kazi lakini ilitumiwa tangu zamani kwa mapambo au kwa vyombo vya thamani katika utumishi wa kidini au wa kifalme.

Kwa sababu ya kuwa metali haba ilitumiwa kama pesa.


Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]