Metali adimu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Metali adimu katika Mfumo radidia wa elementi za kikemia:
H He
Li Be B C N O F Ne
Na Mg Al Si P S Cl Ar
K Ca Sc Ti V Cr Mn Fe Co Ni Cu Zn Ga Ge As Se Br Kr
Rb Sr Y Zr Nb Mo Tc Ru Rh Pd Ag Cd In Sn Sb Te I Xe
Cs Ba * Hf Ta W Re Os Ir Pt Au Hg Tl Pb Bi Po At Rn
Fr Ra ** Rf Db Sg Bh Hs Mt Ds Rg
 
* La Ce Pr Nd Pm Sm Eu Gd Tb Dy Ho Er Tm Yb Lu
** Ac Th Pa U Np Pu Am Cm Bk Cf Es Fm Md No Lr

Metali adimu ni metali zenye tabia ya kutomenyuka kirahisi. Haziguswi na maji au oksijeni za hewa tofauti na metali nyingi. Mara nyingi hutazamiwa kuwa metali za thamani kwa sababu zinadumu na kuwa haba.

Mifano yake ni dhahabu (auri), fedha (ajenti), shaba (kupri), tantali, platini, paladi na rhodi. Kuhusu shaba maoni hutofautiana kama inahesabiwa humo.

Elmenti sintetiki za Bohri, Hassi, Meitneri, Darmstati na Roentgeni zatazamiwa pia kama metali adimu hata kama hazina matumizi kutokana maisha mafupi ya elementi hizi.

Matumizi ya metali adimu[hariri | hariri chanzo]

Metali adimu hasa dhahabu na fedha zilitumiwa kwa mapambo ya thamani kwa watu. Katika utamaduni mbalimbali dhahabu ilikuwa metali ya mfalme au mwene.

Zilifaa pia kwa biashara kwa sababu zilitafutwa na watu kote zikabebwa kirahisi na kudumu. Hivyo vipande vya metali hizi vilipimwa kufuatana uzito na kutumiwa kwa biashara. Baadaye vipande vyenye uzito maalumu viligongwa mhuri na kuwa chanzo cha pesa.

Metali adimu zote (isipokuwa elementi sintetiki)