Thamani

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Thamani (kutoka neno la Kiarabu) ni kiasi gani kitu kinafaa. Mara nyingi njia bora ya kupata thamani ya kitu ni kutumia bei ambayo inaweza kuuzwa. Hata hivyo, Oscar Wilde aliandika kuwa 'watu wanajua bei ya kila kitu lakini hawajui thamani' - kwa maneno mengine thamani ya kweli haitegemei fedha peke yake.

Katika hesabu, thamani ni namba ambayo ni halisi, kitu ambacho kila mtu anaweza kukubaliana nacho. Hata hivyo watu wanaweza kutokubaliana juu ya thamani ya maji, kulingana na kwamba wanaishi jangwani au karibu na mto. Kutokubaliana juu ya thamani ya vitu kunaweza kuunda mapambano kati ya mataifa, vyama vya siasa, dini, n.k.

Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Thamani kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.