Nenda kwa yaliyomo

Kano

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mji wa Kano nchini Nigeria
Jimbo la Kano, barabara huko Kano
Jimbo la Kano, barabara huko Kano

Kano ni mji mkubwa wa tatu nchini Nigeria na makao makuu ya jimbo la kujitawala la Kano. Kuna wakazi 3,626,204.

Kano ni kitovu cha kiuchumi na kiutamaduni ya kaskazini ya Nigeria. Viwanda mbalimbali vinashughulika mazao ya karanga. Kuna uwanja wa ndege wa kimataifa na kituo cha reli kwenda Lagos kupitia Kaduna.

Chuo Kikuu cha Bayero kinaendeleza utamaduni wa utaalamu mwenye historia ndefu mjini uliokuwa mnara wa elimu ya kiislamu tangu karne nyingi.

Kihistoria mji ulikuwa mji mkuu wa usultani wa Kano na kitovu cha Kiislamu katika kanda ya Sahel. Kanu iliundwa kama mji wa Wahausa takriban miaka 1000 iliyopita. Mji ulitajirika kutokana na biashara ya misafara katika Sahel na kuwa mji mkuuwa Usultani. Hadi leo geti mablimbali ya ukuta wa mji wa kale zinasimama. Katika karne ya 19 kiongozi mwislamu wa Kifulani Usman dan Fodio alifanyia Kano vita ya jihadi akimwondoa mtawala wa Kihausa na kuacha Wafulani kama Maamiri.

Kuja kwa Waingereza tangu 1903 kulimfanya Amiri wa Kano mtawala wa nchi lindwa chini ya usimamizi wa Waingereza lakini ni kuundwa kwa nchi ya Nigeria tu kulikomaliza Kano kama nchi ya pekee. Amiri wa Kanu anaendelea kuwa kiongozi wa kiutamaduni anayeheshimiwa. Kitovu cha kiutawala cha kaskazini kilipewa Kaduna lakini katika muundo wa shirikisho Kano imekuwa tena jimbo la kujitawala.

Idadi kubwa ya wakazi ni Waislamu. Uchumi na nafasi za kazi zimevuta pia watu kutoka majimbo waliohamia Kanu. Kuwepo kwa Wakristo mjini kulisababisha mara kadhaa ghasia dhidi yao ambamo mamia waliuawa.

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]