Nigeria

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Federal Republic of Nigeria
Shirikisho la Jamhuri ya Nigeria
Bendera ya Nigeria Nembo ya Nigeria
Bendera Nembo
Kaulimbiu ya taifa: Unity and Faith, Peace and Progress (Umoja na Imani, Amani na Maendeleo)
Wimbo wa taifa: Arise O Compatriots, Nigeria's Call Obey (Amkeni wananchi, mtieni wito la Nigeria)
Lokeshen ya Nigeria
Mji mkuu Abuja
9°10′ N 7°10′ E
Mji mkubwa nchini Lagos
Lugha rasmi Kiingereza
Serikali
Rais
Makamu wa Rais
Shirikisho la Jamhuri
Muhammadu Buhari
- -
Uhuru
kutoka Uingereza
1 Oktoba 1960
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
923,768 km² (ya 31)
1.4%
Idadi ya watu
 - 2005 kadirio
 - 1991 sensa
 - Msongamano wa watu
 
131,530,000 (ya 9)
88,992,220
142/km² (ya 53)
Fedha Naira (₦) (NGN)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
(UTC+1)
(UTC+2)
Intaneti TLD .ng
Kodi ya simu +234

-Nigeria (kisw. pia: Nijeria au Naijeria) ni nchi ya Afrika ya Magharibi kwenye pwani la Bahari Atlantiki. Imepakana na Benin, Niger, Chad na Kamerun. Mji mkuu tangu ni Abuja ikitanguliwa na Lagos hadi mwaka 1991. Nigeria imepata uhuru wake mwaka 1960 ni nchi ya Afrika yote yenye watu wengi.

Jiografia[hariri | hariri chanzo]

Nigeria inaunganisha maeneo tofauti sana ikiwa na msitu wa mvua katika kusini kupitia nchi ya savana hadi kanda ya Sahel na mwanzo wa jangwa la Sahara kaskazini kabisa. Mlima wa juu ni Chappal Waddi yenye 2,419 m juu ya UB.

Hali ya hewa ni ya kitropiki. Kusini kuna mvua mwaka wote lakini kaskazini ya nchi kuna ukame kati ya Novemba na Aprili.

Mito mikubwa ni mto Niger na mto Benue; yote miwili inakutana na kuishia katika delta ya Niger ambayo ni kati ya delta kubwa zaidi duniani.

Mji mkubwa ni Lagos (mji mkuu wa zamani); kati ya miji mingini ni Abuja, Kano, Ibadan, Oshogbo, Ilorin, Abeokuta, Ogbomosho na Port Harcourt.

Nigeria - Majimbo ya shirikisho na nchi jirani

Majimbo ya shirikisho[hariri | hariri chanzo]

Muundo wa Nigeria ni Shirikisho la Jamhuri. Katiba ya nchi imefuata mfano wa katiba ya Marekani. Rais huchaguliwa na wananchi wote ndiye mkuu wa serikali. Anawajibika mbele ya bunge yenye vitengo viwili: Senati na Baraza la Wawakilishi.

Kisiwa cha Lagos, mbele wangwa

Wakazi[hariri | hariri chanzo]

Nigeria hukadiriwa kuwa na wakazi takriban milioni 130. Vikundi vikubwa katika jumla la makabila 300 ni Wahausa na Wafula katika kaskazini (jumla 20-30%), Waigbo (Waibo) katika kusini (14-18%), Wayoruba katika sehemu za magharibi (20-27%). Makadirio ya idadi yanatofautiana sana ni vigumu kupata namba halisi kwa sababu ya umuhimu wake wa kisiasa.

Katika miji mikubwa watu kukaa kwa mchanganyiko wa makablia. Nigeria iliona mara kadhaa vurugo na mapambano kati ya makabila yaliyoongezewa ukali kwa sababu mara nyingi ukabila unaendelea sambamba na tofauti za dini. Watu wa Kaskazini ni zaidi Waislamu na watu wa kusini zaidi Wakristo.

Dini[hariri | hariri chanzo]

Kuthebitisha idadi ya wafuasi wa dini mbalimbali ni vigumu vilevile. Kwa ujumla kaskazini ya nchi ina historia ndefu ya Uislamu na wakazi ni Waislamu hasa Wahaussa. Kusini kuna Wakristo wengi, Waigbo ni zaidi Wakatoliki na Yoruba zaidi Waprotestant. Wengine wanasema ya kwamba idadi za Wakristo na za Waislamu zinalingana - wengine wanaona Waislamu ni wengi kidogo labda 50%, Wakristo 40% na wafuasi wa dini za jadi takriban 10%.

Tangu 1999 swali la sharia au sheria za Kiislamu limeleta utata na mapambano katika majimbo kadhaa. Jimbo la Zamfara linalokaliwa hasa na Wahausa ambao ni Waislamu liliamua kuwa na sharia kama sheria ya kijimbo mwaka 1999 na majimbo mengine yalifuata. Kwa sasa ni Kano, Katsina, Niger, Bauchi, Borno, Kaduna, Gombe, Sokoto, Jigawa, Yobe na Kebbi. Kanuni za sharia hazitumiwi kwa namna moja kati ya majimbo haya; mapambano yalitokea juu ya swali jinsi gani sharia inaathiri raia wasio Waislamu.

Olusegun Obasanjo Rais wa Nigeria 1999 - 2007

Historia[hariri | hariri chanzo]

Kabla ya ukoloni eneo la Nigeria ilikuwa na falme mbalimbali. Kaskazini ilikuwa chini ya sultani za Kiislamu za Kano na Sokoto; kusini ilikuwa na falme za Benin, Ife na Oyo. Kwa jumla eneo la Nigeria haikuwahi kuwa pamoja kabla ya kuja kwa wakoloni waliochora mipaka yao bila kujali mno tamaduni za wenyeji. Ilikuwa azimio la Uingereza kuunganisha maeneo yenye utamaduni na historia tofauti kuwa koloni moja.

Nigeria ilipata uhuru wake tarehe 1 Oktoba 1960 kutoka kwa Uingereza.

Kati ya 1967-1970 nchi iliona vita ya wenyewe kwa wenyewe; magharibi ya nchi inayokaliwa na Waigbo hasa ilijaribu kujitenga wa jina la Biafra wakipinga utawala wa wanajeshi Waislamu. Takriban watu milioni 2 walikufa na njaa wakati ule.

Nigeria iliendelea kuvurugika na mapinduzi ya kijeshi. Tangu miaka ya 1970 Nigeria ilikuwa na mapato makubwa kutokana na mafuta yaliyotolewa kutoka ardhi yakwe hasa katika delta ya mto Niger. Ulaji rushwa na ufisadi wa watawala wa kijeshi ulizuia maendeleo ya nchi jinsi ilivyoonekana katika nchi nyingine yenye mafuta.

Tangu 1999 nchi ilirudi kwa utawala wa kisheria ikapata katiba mpya na kumchagua rais Olusegun Obasanjo aliyerudishwa madarakani mara moja. Majaribio ya wafuasi wake wa kubadilisha katiba na kumpa kipindi cha tatu yameshindikana bungeni. Katika uchaguzi wa mwaka 2007 alishinda Umaru Yar’Adua kwa asilimia 70 za kura. Baada ya kungonjeka kwake makamu wa rais Goodluck Jonathan alichukua madaraka ya urais kuanzia mwaka 2010 akachaguliwa kuwa rais kwenye kura ya 2011. Mwaka 2015 alishindwa katika uchaguzi mkuu na mgombea mwenzake Muhammadu Buhari.

Tangu mwaka 2009 uasi wa kundi la Boko Haram ulivurugisha amani nchini Nigeria. Wanamigambo ya kundi hili wanaotazamiwa kuwa magaidi na Wanigeria wengi walianza kutwaa mamlaka juu ya sehemu za nchi hasa katika mazingira ya jimbo la Borno, kuua wananchi wengi, kuchukua wateka na kupigana na jeshi la Nigeria na nchi jirani. Kutofaulu kwa jeshi la taifa kumaliza ghasia ilikuwa sababu muhimu ya kushindwa kwa rais Jonathan kwenye uchaguzi wa mwaka 2015.

Jeshi[hariri | hariri chanzo]

Jeshi ya Nigeria lina jukumu ya kulinda Jamhuri ya Shirikisho ya Nigeria, kukuza maslahi ya usalama wa kimataifa ya Nigeria , na kuunga mkono juhudi za kulinda amani hasa katika Afrika Magharibi. Jeshi ya Nigeria ya Jeshi la Ardhi, ni Jeshi la Wanamaji na Jeshi la Anga. Jeshi nchini Nigeria limecheza jukumu kubwa katika historia ya nchi tangu uhuru. Junta mbalimbali zilikamata udhibiti wa nchi na zilitawala kupitia wengi wa historia yake. Kipindi cha mwisho cha utawala kilimalizika mwaka 1999 kufuatia kifo cha ghafla cha dikteta wa zamani Sani Abacha mwaka 1998, na mrithi wake, Abdulsalam Abubakar, kumpa mamlaka ya serikali Olusegun Obasanjo aliyechaguliwa kidemokrasia mwaka wa 1999. Ikuchukua faida ya jukumu lake kama nchi yenye wakazi wengi wa Afrika, Nigeria imeweka jeshi lake kama kikosi cha kulinda amani Afrika. Tangu mwaka 1995, jeshi ya Nigeria kupitia mamlaka ya ECOMOG wametumwa kama walinzi wa amani katika Liberia (1997), Ivory Coast (1997-1999), Sierra Leone 1997-1999, [39] na kwa sasa katika mkoa wa Darfur huko Sudan chini ya Umoja wa Afrika.

Angalia pia[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu: 
Majimbo ya Nigeria
Flag of Nigeria.svg
Abia | Abuja Federal Capital Territory | Adamawa | Akwa Ibom | Anambra | Bauchi | Bayelsa | Benue | Borno | Cross River | Delta | Ebonyi | Edo | Ekiti | Enugu | Gombe | Imo | Jigawa | Kaduna | Kano | Katsina | Kebbi | Kogi | Kwara | Lagos | Nasarawa | Niger | Ogun | Ondo | Osun | Oyo | Plateau | Rivers | Sokoto | Taraba | Yobe | Zamfara


Nchi za Afrika Bara la Afrika
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad | Cote d'Ivoire | Eritrea | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Jibuti | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesoto | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Sudan Kusini | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Uhabeshi | Uswazi | Zambia | Zimbabwe
Maeneo ya kiafrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika
Ufaransa: Mayotte · Réunion | Hispania: Visiwa vya Kanari · Ceuta · Melilla | Ureno: Visiwa vya Madeira | Uingereza: · Kisiwa cha St. Helena · Kisiwa cha Diego Garcia
Flag-map of Nigeria.svg Makala hii kuhusu maeneo ya Nigeria bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Nigeria kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.