Lagos

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Lagos inavyoonekana kutoka bandari yake

Lagos ni mji mkubwa wa Nigeria. Ilikuwa mji mkuu wa nchi hadi 1991. Ikiwa na wakazi takriban milioni 9 katika eno la jiji na milioni 12 - 15 katika rundiko la mji ni kati ya miji mikubwa zaidi ya Afrika; inaweza kuwa na nafasi ya pili baada ya Cairo.

Jiografia[hariri | hariri chanzo]

Lagos iko mwambaoni wa Ghuba ya Guinea; wenyeji hutofautiana sehemu mbili kuu ambazo ni "kisiwa" (The Island) na "bara" (Mainland).

Lagos kisiwani[hariri | hariri chanzo]

Lagos kisiwani ni zaidi ya kisiwa kimoja, jina hili linajumlisha pande zote zilizotengwa na bara kwa mfereji ambao ni mlango wa wangwa wa Lagos kwenda baharini.

Visiwa vikubwa ni Lagos Island, Ikoyi, and Victoria pamoja na visiwa vidogo mbalimbali, mara nyingi mifereji midogo kati yao imeshafunikwa kwa majengo na madaraja mengi au kujazwa. Sehemu hii ni kitovu cha biashara na maofisi pamoja na makazi yenye bei za juu.

Madaraja matatu makubwa huunganisha sehemu ya kisiwani na bara ambazo ni madaraja ya Carter, Eko na daraja la tatu la bara.

Ramani ya eneo la Lagos

Historia[hariri | hariri chanzo]

Lagos ilianzishwa kama kijiji cha Wayoruba ikaendelea kukua kutokana na na biashara, bandari yake na kipindi kama mji mkuu wa Nigeria. Nafasi ya mji mkuu ilichukuliwa na Abuja lakini hadi leo Lagos inaendelea kuwa mji mkuu wa biashara na uchumi nchini.

Inaaminiwa ya kwamba Kisiwa cha Lagos kilikaliwa na wavuwi na wakulima Wayoruba tangu karne ya 14. Katika karne ya 15 eneo lilikuwa kwa muda chini ya ufalme wa Benin. Wakati ule lilitwa "Eko".

Mwaka 1472 mbaharia Mreno Ruy de Sequeira alifika Eko akaanzisha kituo cha biashara lililoitwa "Lagos" - kwa Kireno neno hili lamaanisha "maziwa" ni pia jina la mji Lagos katika Ureno ya kusini. Katika karne zilizofuata Lagos pamoja na utajiri wa Oba ilikua kutokana na bishara ya watumwa.

Katika karne ya 19 Waingereza walijaribu kukandamiza biashara hii ya watumwa katika Afrika ya Mashariki . 1841 Oba mpya aliyeitwa Akitoye alipiga biashara ya watumwa marufuku lakini alipinduliwa kwa sababu ya upinzani wa wafanyabiashara wenyeji. Akitoye aliomba usaidizi wa Uingereza. Manowari za kiingereza walishambulia Lagos tar. 26 na 27 Desemba 1852 na kumrudisha mfalme. Matatizo ya biashara ya watumwa yaliendelea na Waingereza walichukua kisiwa cha Lagos na kuifanya kwanza eneo lindwa halafu koloni. Oba alibaki na madaraka machache.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]


Kujisomea[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]


WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:


Flag-map of Nigeria.svg Makala hii kuhusu maeneo ya Nigeria bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Lagos kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.