Nenda kwa yaliyomo

Afrika ya Mashariki

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
      Eneo la Afrika Mashariki kulingana
na Umoja wa Afrika
Ramani ya Afrika Mashariki kadiri ya Umoja wa Mataifa.

Afrika ya Mashariki ni sehemu ya bara la Afrika ambayo iko upande wa mashariki, ikipakana na Bahari ya Hindi. Kadiri ya Umoja wa Mataifa,Inajumuisha Pembe ya Afrika upande wa juu na Afrika Kusini-Mashariki upande wa chini na Maeneo ya visiwa. Inajulikana kuwa na Bonde la ufa ,Maziwa kuu ya Afrika, Milima mikubwa zaidi Afrika na mandhari ya Savannah na Safari ambayo ni vivutio kwa watalii.

Nchi

Afrika ya Mashariki ina nchi zifuatazo:

Bendera Nchi Mji Mkuu Idadi ya Watu Mji Mkubwa Lugha Rasmi Eneo (km²) Msongamano (kwa km²)
Burundi Gitega 13,689,450 Bujumbura Kirundi, Kifaransa 27,834 492
Komori Moroni 880,000 Moroni Kikomori, Kiarabu, Kifaransa 1,861 473
Jibuti jibuti 1,094,000 Jibuti Kifaransa, Kiarabu 23,200 47
Eritrea Asmara 3,600,000 Asmara Kitigrinya, Kiarabu, Kiingereza 117,600 31
Ethiopia Addis Ababa 128,691,692 Addis Ababa Kiamhari 1,104,300 117
Kenya Nairobi 55,339,003 Nairobi Kiingereza, Kiswahili 580,367 95
Madagascar Antananarivo 31,195,932 Antananarivo Kimalagasi, Kifaransa 587,041 53
Malawi Lilongwe 21,104,482 Blantyre Kiingereza, Chichewa 118,484 178
Morisi Port Louis 1,289,000 Port Louis Kiingereza 2,040 632
Msumbiji Maputo 33,635,160 Maputo Kireno 801,590 42
Rwanda Kigali 13,954,471 Kigali Kinyarwanda, Kiingereza, Kifaransa 26,338 530
Shelisheli Victoria 100,000 Victoria (Shelisheli) Krioli ya Shelisheli, Kiingereza, Kifaransa 455 220
Somalia Mogadishu 18,358,615 Mogadishu Kisomali, Kiarabu 637,657 29
Sudan Khartoum 50,042,791 Omdurman Kiarabu, Kiingereza 1,861,484 27
Sudan Kusini Juba 11,730,000 Juba Kiingereza 619,745 19
Tanzania Dodoma 66,617,606 Dar es Salaam Kiswahili, Kiingereza 945,087 71
Uganda Kampala 48,656,601 Kampala Kiingereza, Kiswahili 241,550 201
Bendera Nchi Mji Mkuu Idadi ya Watu Mji Mkubwa Lugha Rasmi Eneo (km²) Msongamano (kwa km²)
Zambia Lusaka 20,723,965 Lusaka Kiingereza 752,618 28
Zimbabwe Harare 16,340,822 Harare Kiingereza, Shona, Ndebele 390,757 42
Mayotte Mamoudzou 320,901 Mamoudzou Kifaransa 374 776
Réunion Saint-Denis 878,591 Saint-Denis Kifaransa 2,512 0.890
  • Mayotte na Réunion, zilizokuwa makoloni na sasa ni mikoa ya Ufaransa, zinahesabiwa pia katika orodha hii.

Hata hivyo:

Tazama pia

Historia

Afrika ya Mashariki inatajwa na sayansi kuwa mahali ambako watu wa kwanza duniani walikopatikana.

Majina ya miji ya Afrika ya Mashariki imetajwa mara ya kwanza katika Periplus ya Bahari ya Eritrea (karne ya 1 B.K.).

Tangu uenezaji wa ukoloni wa Kizungu upande wa Mashariki wa bara ulianza kuitwa Afrika ya Mashariki. Somalia, Eritrea na Ethiopia za leo zilitawaliwa na Italia kama "Afrika ya Mashariki ya Kiitalia" (Africa Orientale Italiana) katika miaka ya 1936 hadi 1941, Kenya ilitwaliwa na Uingereza kwa jina la "Afrika ya Mashariki ya Kiingereza" (East Africa Protectorate au pia British East Africa) hadi 1920, Tanganyika pamoja na Rwanda na Burundi zilijulikana kama "Afrika ya Mashariki ya Kijerumani" (Deutsch Ostafrika) hadi 1919 na Msumbiji iliitwa mara nyingi "Afrika ya Mashariki ya Kireno" (África Oriental Portuguesa) hadi uhuru.

Lugha

Wakazi wengi wa Afrika ya Mashariki ni wasemaji wa lugha za Kibantu; sehemu ya kaskazini wasemaji wa lugha za Kihamiti ni wengi (Waoromo, Wasomalia). Katika Ethiopia kuna wasemaji wengi wa lugha za Kisemiti. Pia kuna wasemaji wa lugha za Kiniloti na lugha za Khoisan.

Ushirikiano

Nchi mashuhuri zaidi katika sehemu hii ni Kenya, Uganda, Tanzania, Rwanda na Burundi kwa sababu ya kutumia lugha moja katika mawasiliano baina ya wananchi wa sehemu hii, yaani Kiswahili.

Aghalabu nchi za Afrika ya Mashariki zinazungumza lugha ya Kiswahili kama lugha ya mawasiliano kati yao, kwani katika nchi hizi kuna makabila mengi sana na kila kabila lina lugha yake ambayo kawaida inatumika nyumbani baina ya watu wa kabila moja, lakini wakitaka kuwasiliana na makabila mengine, mara nyingi hutumia lugha ya Kiswahili, na hii ni kwa sababu lugha hii ndiyo iliyoenea zaidi na kufahamika zaidi katika eneo hili la dunia.

Nchi za Afrika ya Mashariki, hasa Kenya, Uganda na Tanzania ni nchi ambazo ni karibu tangu zamani. Zimeshirikiana historia, zote zimekaliwa hasa na makabila yanayotumia lugha za Kibantu (Kenya na Uganda wana pia idadi muhimu ya wakazi wasiotumia lugha za Wabantu). Katika nchi zote tatu lugha ya Kiswahili imekuwa lugha muhimu ingawa kwa daraja mbalimbali. Wakati wa ukoloni zilitawaliwa na Uingereza iliyoacha taasisi na taratibu mbalimbali zilizosaidia kuanzishwa kwa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki wakati wa uhuru.

Tanzania, Kenya na Uganda zina ukubwa wa eneo la maili za mraba; Tanzania 360,000 ikifuatiwa na Kenya 224,960 na Uganda 93,980 upande wa mashariki nchi hizi zimepakana na bahari ya Hindi na upande wa kaskazini mashariki zimepakana na Somalia, upande wa kaskazini zimepakana na Ethiopia na Sudan Kusini upande wa magharibi ni Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na jamuhuri ya Rwanda na Burundi, kusini ni Zambia, Malawi na Msumbiji.

Nchi hizi zimepitiwa na mstari wa ikweta, umepita Kenya na kusini mwa Uganda. Kenya na Tanzania zina ukanda wa pwani wenye bandari za Mombasa; Tanga; Bagamoyo; Dar es Salaam; Zanzibar; Kilwa na Mtwara.


Nchi za Afrika Bara la Afrika
Afrika ya Kati (Jamhuri ya) | Afrika Kusini | Algeria | Angola | Benin | Botswana | Burkina Faso | Burundi | Cabo Verde | Chad | Cote d'Ivoire | Eritrea | Eswatini | Ethiopia | Gabon | Gambia | Ghana | Guinea | Guinea Bisau | Guinea ya Ikweta | Jibuti | Kamerun | Kenya | Komori | Kongo (Jamhuri ya) | Kongo (Jamhuri ya Kidemokrasia ya) | Lesotho | Liberia | Libya | Madagaska | Malawi | Mali | Misri | Morisi (Visiwa vya) | Mauritania | Moroko | Msumbiji | Namibia | Niger | Nigeria | Rwanda | Sahara ya Magharibi | Sao Tome na Principe | Senegal | Shelisheli | Sierra Leone | Somalia | Sudan | Sudan Kusini | Tanzania | Togo | Tunisia | Uganda | Zambia | Zimbabwe
Maeneo ya Afrika ambayo ni sehemu za nchi nje ya Afrika
Hispania: Kanari · Ceuta · Melilla | Italia: Pantelleria · Pelagie | Ufaransa: Mayotte · Réunion | Uingereza: · St. Helena · Diego Garcia | Ureno: Madeira