Nenda kwa yaliyomo

Harare

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Harare inavyoonekana kutoka kilima cha Kopje
Map of Zimbabwe with the province highlighted
Map of Zimbabwe with the province highlighted

Harare (zamani: Salisbury) ni mji mkuu wa Zimbabwe pia mji mkubwa nchini ukiwa kitovu cha utawala na uchumi. Uko kwenye kimo cha mita 1,500 juu ya UB.

Idadi ya wakazi imehesabiwa kufika 1,492,000[1], pamoja na mitaa ya nje hadi 3,120,000. Mtaa wa nje ulio mkubwa ni Chitungwiza yenye wakazi 340,000 kusini kwa uwanja wa ndege wa kimataifa.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Mji ulianzishwa mwaka 1890 BK kama kambi la jeshi la binafsi la Cecil Rhodes. Tangu kuwa makao ya kudumu mji ulipewa jina la Salisbury kutokana na Lord Salisbury aliyekuwa waziri mkuu wa Uingereza miaka ile akamsaidia Cecil Rhodes kazika mipango yake ya kupanusha ukoloni katika Afrika ya Kusini. Salisbury ilipata cheo cha mji mwaka 1935 ikawa mji mkuu wa Maungano ya Rhodesia na Unyasa mwaka 1953 hadi 1963.

Baada ya uhuru wa Zimbabwe jina la Salisbury ilibadilishwa mwaka 1982 kwa heshima ya chifu wa Washona Neharawa kuwa Harare.

Tangu 2002 mji uliathiriwa vibaya na matatizo ya kisiasa nchini Zimbabwe. Vyama vya upinzani vilipata kura nyingi mjini kushinda serikali ya Robert Mugabe katika chaguzi za kisiasa. Serikali ikalipiza kisasi kwa kufuta Halmashauri ya Mji. Mwaka 2005 serikali ilibomoa mitaa ya vibanda katika kempeni ya Operation Murambatsvina (Mradi wa "kuondoa takataka"). Lakhi za watu walifukuzwa katika nyumba zao na biashara zao zikabomolewa. Wapinzani waliona kampeni hii kama jaribio la kupunguza idadi ya wafuasi wao katika mji mkuu.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Harare kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.