Bulawayo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Bendera ya Bulawayo
Mahali pa Bulawayo
"Picha hii ilipigwa wakati wa ziara ya Bulawayo, Rhodesia, sasa Zimbabwe, na watu wawili ambao baadaye walitibiwa ugonjwa wa Marburg. Picha hii ilipigwa Februari 2 au 3, 1975, usiku wa pili au wa tatu baada ya mgonjwa wa virusi vya Marburg #1 kufika. kuwasiliana na vekta isiyojulikana."

Bulawayo ni mji mkubwa wa pili wa Zimbabwe wenye wakazi 676,787 (sensa ya 2002). Iko kusini-magharibi ya nchi hiyo, katikati ya Matabeleland.

Jina la mji linatokana na neno la Kindebele "Kwabulawayo" yaani "machinjoni". Mji wa leo ulijengwa juu ya mabaki ya boma la mfalme Lobengula. Lobengula aliwahi kujenga boma lake la kwanza 1871 takriban kilomita 15 kusini ya mji. 1881 alihamia penye mji wa sasa.

1893 ufalme wa Lobengula ulishambuliwa na jeshi la Cecil Rhodes na mfalme aliamua kuchoma boma lake alipoona alishindwa kuzuia maadui. Waingereza walianzisha mji wao juu ya mabaki ya makazi ya awali. 1897 ilipewa cheo cha manisipaa na kuungwa na reli.

Wakazi walio wengi ni Wandebele.

Bulawayo ilikuwa mji ambako upinzani dhidi ya ukoloni ulianza. Leo hii ni kitovu cha upinzani dhidi ya serikali ya Robert Mugabe.