Ukoloni

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Ramani ya ukoloni duniani mwishoni mwa Vita Kuu ya Pili ya Dunia mwaka 1945.

Ukoloni ni mfumo wa taifa moja kuvuka mipaka yake na kutawala maeneo ya mbali yanayokaliwa na watu wengine kwa nyanja za kiuchumi, kiutamaduni na kijamii. Maeneo haya yanaweza kuitwa koloni au eneo lindwa.

Ukoloni unaitwa hasa kipindi tangu karne ya 15 ambako Ureno na Hispania zilianza kuenea Afrika na Amerika ya Kusini na kudumu hadi baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia. Lakini kulikuwa na vipindi vya ukoloni pia zamani katika historia kama vile ukoloni wa Roma ya Kale, ukoloni wa Waarabu na vingine. Ukoloni kwa maana hii inaweza kuwa tofauti na kuundwa kwa koloni katika vipindi mbalimbali vya historia ambako maeneo bila wakazi au penye wakazi wachache sana yaliingiliwa na watu kutoka sehemu nyingine.


Nchi za Afrika ziliwekwa chini ya ukoloni wa nchi za Ulaya mara baada ya Mkutano wa Berlin wa 1885 ulioitishwa na chansella wa Ujerumani Bismarck mwaka 1884-1885.

Nchi zilizojenga ukoloni huu wa Afrika zilikuwa Uingereza, Ufaransa, Ureno, Ujerumani, Uhispania, Italia na Ubelgiji.

Ukoloni mamboleo ni aina ya nchi au kundi la nchi fulani kutawala nchi nyingine kinyemela kwa kuweka vikwazo na masharti yatakayowafanya watawaliwa waendelee kuwa na uchumi tegemezi ili wawatajirishe zaidi hao wanaowatawala kinyemela

Utawala wa kikoloni[hariri | hariri chanzo]

Utawala wa kikoloni ni utawala ulioanzishwa hasa na Wazungu kwa lengo la kunyonya na pengine kuwabagua Waafrika na watu wengine wenyeji wa Asia, Oseania na Amerika.

Utawala huo ulitegemea hali ya taifa lenyewe lililohusika pamoja na hali ya jamii zilizokuwa zinatawaliwa.

Baada ya kuanzisha utawala huo wakoloni walibadilisha utawala wa jadi na kuufanya utawale kwa masilahi ya wakoloni; pia utawala huo uliharibu hadhi ya utawala wa jadi na misingi ya jadi.

Muundo wa utumishi[hariri | hariri chanzo]

Muundo wa utumishi katika utawala wa kikoloni ulikuwa wa kibaguzi na kinyonyaji:

(a) Kazi katika ngazi za juu zilifanywa na Wazungu, hasa kazi zilizohitaji ujuzi.

(b) Kazi katika ngazi za chini zilifanywa na wenyeji kama vile ukarani, utarishi, ufagizi na ukorokoroni.

(c) Wakoloni walitoa elimu duni kwa wenyeji ili waendelee kuwaajiri katika ngazi za chini.

Makoloni yaliyokuweko Afrika[hariri | hariri chanzo]

1. Ubelgiji ilikuwa na Kongo, Burundi, Rwanda, Zaire (formerly the Congo)

2. Uingereza ilikuwa na Botswana, Cameroon, Egypt, Gambia, Ghana, Kenya, Lesotho, Malawi, Mauritius, Nigeria, Seychelles, Sierra Leone, Somalia, South Africa, Sudan, Swaziland, Uganda, Zanzibar, Zambia, Zimbabwe Same. With the addition of Eritrea from 1943 until the United Nations returned it to Ethiopian sovereignty as an independent, autonomous unit in 1952. Libya (with France) from 1943 to its independence in1952. Also, the new territory of Tanzania which was a uniting of Tanganyika and Zanzibar in 1964.

3. Ufaransa ilikuwa na Algeria, Benin, Central African Republic, Chad, Comoros, Cote D'Ivoire, Djibouti, Gabon, Guinea, Madagascar, Mali, Mauritania, Morocco, Niger, Senegal, Tunisia Same. Cameroon, Libya (with Britain) from1943 to its independence in 1952

3. Ujerumani ilikuwa na Burundi, Cameroon, Germany, Morocco, Namibia, Rwanda, Tanganyika, Togo

4. Italia ilikuwa na Libya (by conquest in 1911. Libya was previously ruled by Turkey form the 16th century until the Italian invasion) Eritrea (by invasion) 1936-1941. After World War II, no countries .

5. Uholanzi ilikuwa na South Africa

8. Ureno ilikuwa na Angola, Cape Verde, Guinea-Bissau, Mozambique, San Tome & Principe

7. Hispania ilikuwa na Equatorial Guinea, Morocco".

Vitabu[hariri | hariri chanzo]