Vita ya Miaka Saba

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Maeneo yote yaliyoathiriwa na Vita ya Miaka Saba      Uingereza, Prussia, Ureno na nchi ndogo      Ufaransa, Hispania, Austria, Urusi, Uswidi, pamoja na koloni na nchi ndogo upande wao

Vita ya Miaka Saba ilitokea kati ya miaka 1756 hadi 1763. Ilitokana na mashindano ya nchi za Ulaya ikasambaa pande nyingi za dunia. Hivyo imeitwa "Vita Kuu ya Dunia" ya kwanza hata kama jina hili kwa kawaida linatumiwa kwa ajili ya vita kati ya 1914 na 1918.

Ushirikiano kati ya nchi za Ulaya mwanzoni wa vita ya miaka 7.

Washiriki[hariri | hariri chanzo]

Washiriki katika vita hii walikuwa nchi za Ulaya na koloni zao pia watu wa sehemu mbalimbali za dunia walioshikamana nao.

Walipopigana walikuwa:

Sababu za vita[hariri | hariri chanzo]

Vita ilianza kwa sababu mbili hasa:

 • ndani ya Amerika ya Kaskazini Ufaransa na Uingereza zilishindana kuhusu upanuzi wa maeneo yao.
 • katika Ulaya Prussia iliwahi kutwaa jimbo la Silesia kutoka Austria na Austria ilitaka kuchukua jimbo hili tena.
 • nchi nyingi za Ulaya ziliogopa uwezo mkubwa mno wa nchi nyingine ikiruhusiwa kushinda vitani hivyo ziliamua kuingilia kati

Mashindano na hofu hizi zilisababisha kutokea kwa makambi haya mawili makubwa.

Vituo vikuu vya Waingereza (nyekundu) na Wafaransa (buluu) katika Uhindi kabla ya vita

Mapigano[hariri | hariri chanzo]

Mapigano yalitokea katika Ulaya hasa Ujerumani, halafu katika Uhindi, Amerika ya Kaskazini, kwenye visiwa vya Karibi, pwani za Afrika na Ufilipino.

 • Uingereza ilitwaa "Ufaransa mpya" au sehemu ya Kifaransa ya Kanada ya leo na kuwafukuwa Wafaransa katika maeneo magharibi ya koloni zao.
 • Katika Karibi Waingereza walitwaa visiwa vingi vya Wafaransa isipokuwa Martinique na Guadeloupe.
 • Katika Uhindi vituo vya Ufaransa vingi vilitwaliwa isipokuwa Pondicherry iliyobaki kama koloni ndogo ya Ufaransa (hadi 1960). Waingereza kwa kutwaa kipaumbele katika Ubengali waliweka msingi wa utawala wao wa baadaye juu ya Uhindi wote.
 • Katika Afrika Waingereza walitwaa kituo cha St. Louis katika Senegal kutoka Ufaransa (ilirudishwa baada ya vita)
 • Prussia iliweza kutetea jimbo la Silesia dhidi ya Austria ikapata sifa nyingi kwa sababu jeshi lake lilishindana na Waaustria, Warusi na Wafaransa wakati mmoja. Lakini mnamo mwaka 1762 nguvu za Prussia zilikwisha ikaelekea kushindwa. Iliokolewa kwa sababu malkia Elizabeth wa Urusi alikufa na mfalme mpya Peter III alimpenda sana mfalme wa Prussia akaamua kupatana naye badala ya kumshambulia tena. Hivyo Austria ilibaki kama adui pekee ikashindwa.
Vita ya miaka 7 katika Amerika ya Kaskazini
buluu: eneo la Kifaransa; nyekundu: eneo la Kiingereza kabla ya vita; Ufaransa ilipoteza yote

Matokeo[hariri | hariri chanzo]

Matokeo makuu ya vita[hariri | hariri chanzo]

 • Uingereza ilikuwa nchi yenye koloni nyingi duniani baada ya Hispania ikaelekea kuipita. Pia ilitawala bahari za dunia kwa kuwa taifa lenye manowari mengi na vituo pamoja na bandari kwenye mabara yote.
 • uwezo wa Ufaransa ulipunguzwa ikipotea koloni zake katika Amerika ya Kaskazini na kubaki na maeneo madogo tu katika Karibi na Uhindi.
 • Prussia ilitoka vitani kama nchi muhimu ya tano ya Ulaya pamoja na Ufaransa, Austria, Uingereza, na Urusi.

Matokeo ya baadaye[hariri | hariri chanzo]

 • Msingi wa Kiingereza kuwa lugha ya kwanza duniani uliwekwa kwa sababu kilitumiwa kote katika koloni za Uingereza
 • Ushindi wa Uingereza ulikuwa msingi wa mapinduzi na uhuru wa Marekani miaka 13 baadaye. Walowezi walijifunza mitindo ya vita waliposhiriki katika vita upande wa Uingereza na walitumia ujuzi huo baadaye dhidi ya Uingereza. Kuondolewa kwa Ufaransa kulipunguza vizuizi dhidi ya upanuzi wa Marekani katika Amerika ya kaskazini.
 • Uadui wa Ufaransa dhidi ya Uingereza ulibaki ukaimarishwa na kusababisha usaidizi wa Ufaransa kwa waasi wa Amerika ya Kaskazini mwaka 1776 hivyo kuzaliwa kwa taifa jipya la Marekani.
 • Kudhoofishwa kwa Ufaransa kwa sababu ya gharama kubwa ya vita na gharama ya kusaidia Wamarekani baadaye uliathiri uchumi na sifa za utawala wa kifalme na kuwa sababu muhimu ya mapinduzi ya Kifaransa
 • Ushindi wa Prussia ulisababisha mashindano ya mfululizo kati ya Prussia na Austria juu ya kipaumbele katika Ujerumani yaliyoonekana baadaye hadi vita ya 1866.

Picha za watawala wa nchi shiriki za Vita ya miaka saba[hariri | hariri chanzo]

Hourglass.svg Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Vita ya Miaka Saba kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.