Nenda kwa yaliyomo

Jimbo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Jimbo ni eneo fulani lililotengwa kwa ajili ya kurahisisha utawala ndani ya dola au nchi fulani. Neno latumiwa pia kwa vitengo mmndani ya Kanisa.

Jimbo la dola

[hariri | hariri chanzo]

Majimbo huwa na madaraka mbalimbali, na mazoea katika matumizi ya neno hili ni tofauti kati ya nchi na nchi.

Mara nyingi jimbo ni eneo lenye kiwango kikubwa cha kujitawala hasa majimbo ndani ya muundo wa shirikisho; mifano michache tu ni majimbo ya Afrika Kusini, Nigeria, Marekani au Ujerumani.

Wakati mwingine jimbo ni jina la kihistoria tu hata halina madaraka ya kiutawala tena.

Jimbo la uchaguzi

[hariri | hariri chanzo]

Jimbo la uchaguzi ni eneo ambako mbunge huchaguliwa. Nchi za Afrika ya Mashariki hugawiwa kwa majimbo ya uchaguzi; katika kila jimbo mwakilishi mmoja huchaguliwa na wananchi kwa njia ya kura atakayekuwa mbunge wa eneo hili katika bunge la kitaifa.

Katika nchi yenye muundo wa shirikisho kina pia majimbo yauchaguzi kwenye ngazi za madola au majimbo ya kujitawala ndani ya taifa.

Jimbo la Kanisa

[hariri | hariri chanzo]

Vilevile ndani ya Kanisa jina linatumiwa tofauti na madhehebu mbalimbali.

  • Jimbo la Kanisa Anglikana ni kitengo cha kujitegemea na kujitawala cha kanisa hili katika nchi fulani kwa mfano Jimbo la Tanzania ambalo linaunganisha dayosisi zote za nchi hiyo. Penye Waanglikana wachache jimbo linaweza kujumlisha wakristo wake katika nchi kadhaa kwa mfano jimbo Anglikana la Afrika ya Kati inaunganisha Botswana, Malawi, Zambia na Zimbabwe.
  • Kwa Walutheri jimbo ni sehemu tu ya dayosisi, ingawa inajumuisha shirika kadhaa.
Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Je, unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.


Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.