Kanisa la Moravian Tanzania

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Mwanakondoo mwenye bendera ya ushindi ni ishara ya Kristo mfufuka na sehemu ya nembo la KMT

Kanisa la Moravian Tanzania (KMT) ni muungano wa majimbo ya Kanisa la Moravian nchini Tanzania. Makao makuu yapo Mbeya mjini. Idadi ya Wakristo ilikadiriwa kuwa 410,000 mnamo mwaka 1998.

Majimbo ya KMT[hariri | hariri chanzo]

Kuna majimbo manne ya KMT ambayo ni

Kila jimbo ni kanisa kamili la kujitegemea.

Pamoja na hayo kuna majimbo matatu ya misioni (misheni) ambayo hayakufikia hali ya kujitegemea kikamilifu bado yakishirikiana kila moja na jimbo mzazi. Haya ni Jimbo la Misioni Mashariki ya Tanzania na Zanzibar (mzazi: Jimbo la Kusini - Rungwe), Kanisa la Moravian Ziwa Tanganyika – Jimbo la Misheni (Mzazi: Jimbo la Magharibi - Tabora) na Jimbo la Misheni Kaskazini (Mzazi: Jimbo la Kusini-Magharibi - Mbeya).

Kwa pamoja KMT inaendesha Chuo Kikuu Teofilo Kisanji na kutoa Kiongozi Kalenda ya Moravian. Kazi nyingine ya pamoja ni kutolewa kwa "Kiongozi Kalenda" ambayo ni chaguo ya maneno ya Biblia kwa kila siku.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Kazi ya Wamoravian ilianza Tanzania mnamo mwaka 1891 wamisionari wa kwanza kutoka Ujerumani walipofika Rungwe katika eneo la Wanyakyusa. Kutoka Unyakyusa kazi ilipanuka kwa kuunda vituo huko Utengule (Mbeya)]] (kwa Wasafwa) na Mbozi (kwa Wanyiha).

Kazi katika magharibi ya nchi ilianza 1897 Wamoravian walipokabidhiwa kituo cha Urambo kilichowahi kuanzishwa na shirika la misioni la London (LMS).

Ndiyo chanzo cha majimbo ya Kusini (Rungwe) na Magharibi (Tabora).

Jimbo la Kusini Magharibi lilitengwa na lile la Kusini mwaka 1976.

Jimbo la Rukwa lilijitegemea na lile la Tabora mnamo 1986.

Hasa katika mkoa wa Mbeya kanisa la Moravian ni kubwa kati ya madhehebu ya Kiprotestanti.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]