Utengule
Utengule ni jina la sehemu tofauti katika kusini ya nchi Tanzania:
- Utengule Usongwe katika wilaya ya Mbeya Vijijini takriban 17 km kutoka Mbeya upande wa kusini-magharibi.
- Utengule Usangu katika wilaya ya Mbarali.
Utengule zote mbili za juu zina uhusiano wa Kihistoria zilikuwa makao makuu ya chifu Merere II wa Wasangu aliyehamisha boma lake 1877 kutoka Usangu kwenda Usafwa kutokana na mashambulio ya Wahehe na kuita boma jipya tena "Utengule"..
Kuna pia
- Utengule (Kilombero) katika Wilaya ya Kilombero, Mkoa wa Morogoro
- Utengule (Makambako) katika wilaya ya Makambako Mjini.