Umisionari

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

Umisionari ni utendaji unaolenga kueneza dini fulani.

Asili ya neno ni missio (kwa Kilatini utume).

Mmisionari au mwanamisheni ndiye mtu anayefanya kazi hiyo, hasa katika maeneo ambayo dini hiyo haipo au haijakua.

Mara nyingi wamisionari wanachangia pia maendeleo ya jamii, hasa kupitia elimu, utabibu, utunzaji wa watoto yatima na walioathiriwa na vita na maradhi.

Pengine uenezaji wa dini unatumia mbinu zisizokubalika kijamii, kama vile kulazimisha kwa namna moja au nyingine mtu asiyetumwa na moyo wake kukubali dini mpya.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Simple English Wiktionary
Wikamusi ya Kiswahili ina maelezo na tafsiri ya maana ya neno: