Nenda kwa yaliyomo

Masiya

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Kristo)
Nabii Samueli akimpaka mafuta kijana Daudi kati ya kaka zake awe mfalme wa Israeli: mchoro huu wa karne ya 3 uko Dura Europos, Syria.
Yesu Kristo
Hukumu ya Mwisho kadiri ya Jean Cousin the Younger (mwisho wa karne ya 16).
Mfululizo wa kurasa juu ya Yesu
Yesu
Yesu Kristo na Ukristo

Umwilisho  • Utoto wa Yesu  • Ubatizo
Arusi ya Kana • Utume wa Yesu • Mifano ya Yesu  • Miujiza ya Yesu
Kugeuka sura • Karamu ya mwisho • Msalaba wa Yesu  • Maneno saba
Kifo cha Yesu  • Ufufuko wa Yesu
Kupaa mbinguni  • Ujio wa pili
Injili  • Majina ya Yesu katika Agano Jipya  • Yesu kadiri ya historia  • Tarehe za maisha ya Yesu • Kristolojia

Mazingira ya Yesu

Wayahudi • Kiaramu • Bikira Maria • Yosefu (mume wa Maria) • Familia takatifu • Ukoo wa Yesu • Ndugu wa Yesu • Yohane Mbatizaji

Mitazamo juu ya Yesu

Mitazamo katika Agano Jipya · Mitazamo ya Kikristo • Mitazamo ya Kiyahudi • Mitazamo ya Kiislamu • Yesu katika sanaa

Masiya (au Masiha), kutoka Kiebrania מָשִׁיחַ, Māšîăḥ mashiakh, maana yake Mpakwamafuta ni jina la heshima ambalo Biblia inampa mfalme au kuhani aliyewekwa wakfu kwa Mungu kwa kupakwa mafuta atende kwa niaba yake kazi ya kusaidia taifa lake hasa kwa kulikomboa.[1]

Tofauti na kawaida, Biblia inamtaja kama Masiha hata mfalme Koreshi Mkuu wa Uajemi kwa sababu Mungu alimtumia kutoa Wayahudi katika uhamisho wa Babeli na kuwaruhusu warudi Yerusalemu na kujenga upya hekalu[2]

Hata hivyo kwa namna ya pekee jina hilo linatumika kwa Mwana wa Daudi, mtawala wa Israeli[3] katika wakati wa mwisho ambao utakuwa wa amani duniani[4]

Katika Ukristo

[hariri | hariri chanzo]

Jina hilo lilitafsiriwa na Septuaginta kwa Kigiriki Χριστός (Khristós)[5] nalo lilitumiwa mapema na Wakristo wa lugha hiyo kwa Yesu wa Nazareth kwa sababu ya kusadiki ndiye mkombozi aliyetimiza kikamilifu kila utabiri wa manabii wa Agano la Kale. Ndiyo sababu jina lake la awali limekuwa linaongezewa kwa kawaida hilo la Kristo, hivi kwamba imezoeleka kumuita Yesu Kristo.

Kwa asili ni tamko la imani lenye sehemu mbili: jina "Yesu" na cheo "Kristo".

Katika lugha ya Kigiriki "Yesu Kristo" mara nyingi ni sentensi kamili, maana yake "Yesu ndiye Masiya wa Mungu", yaani Yesu ndiye Masiya aliyetangazwa na manabii wa Agano la Kale na kutazamiwa na Israeli.

Katika aya nyingine za Agano Jipya "Yesu Kristo" tayari imetumika kama jina (linganisha: rais Mkapa, au: Mkapa rais - si yule Mkapa mwingine...)

Kutokana na umuhimu wa imani hiyo kwa wafuasi wa Yesu[6], wenyewe walianza kuitwa Wakristo huko Antiokia, mji wa kwanza kuwa na waumini wenye asili ya kimataifa na waliozungumza Kigiriki kuliko wale wenye asili ya Kiyahudi. Kumbe katika mazingira ya Kisemiti wanaendelea kuitwa kama awali Manasara, yaani Wanazareti.

Katika Uislamu

[hariri | hariri chanzo]

Hadithi za Uislamu pia zinafundisha kwamba nabii Isa, mwana wa Bikira Mariamu, alikuwa ametabiriwa kama Masih (المسيح) wa Waisraeli, na kwamba atarudi duniani siku ya Kiyama, pamoja na Mahdi, ili kumsinda Masih ad-Dajjal, yaani Mpingakristo.[7]

  1. Kut 30:22-25}}
  2. Jewish Encyclopedia: Cyrus: Cyrus and the Jews: "This prophet, Cyrus, through whom were to be redeemed His chosen people, whom He would glorify before all the world, was the promised Messiah, "the Shepherd of Yhwh" (xliv. 28, xlv. 1)."
  3. Megillah 17b-18a, Taanit 8b
  4. Sotah 9a
  5. Etymology Online
  6. Tunahitaji kujua “habari za Yesu wa Nazareti, jinsi Mungu alivyomtia mafuta kwa Roho Mtakatifu na nguvu” (Mdo 10:38).
  7. "Muttaqun OnLine - Dajjal (The Anti-Christ): According to Quran and Sunnah". Muttaqun.com. Iliwekwa mnamo 9 Novemba 2012.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  • Kaplan, Aryeh. From Messiah to Christ, 2004. New York: Orthodox Union.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mambo ya Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Masiya kama historia yake au athari wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.