Syria

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
الجمهورية العربية السورية
Al-Jumhūriyyah al-ʿArabiyyah as-Sūriyyah

Jamhuri ya Kiarabu ya Syria
Bendera ya Syria (Shamu) Nembo ya Syria (Shamu)
Bendera Nembo
Kaulimbiu ya taifa: --
Wimbo wa taifa: Homat el Diyar
"Walinzi wa nchi"
Lokeshen ya Syria (Shamu)
Mji mkuu Dameski
33°30′ N 36°18′ E
Mji mkubwa nchini Dameski
Lugha rasmi Kiarabu
Serikali Jamhuri
Bashar al-Assad
Muhammad Naji al-Otari
Uhuru
Ilitangazwa (1)
Ilitangazwa (2)
Ilitambuliwa

Septemba 19361
1 Januari 1944
17 Aprili 1946
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
183,885 km² (ya 89)
0.06
Idadi ya watu
 - Julai 2012 kadirio
 - Msongamano wa watu
 
22,530,746[1] (ya 54)
118.3/km² (101)
Fedha Lira ya Shamu (SYP)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
EET (UTC+2)
EEST (UTC+3)
Intaneti TLD .sy
Kodi ya simu +963

-

1 Mkataba kati ya Ufaransa na Syria ya 1936 haikutambuliwa awali na Ufaransa.


Ramani ya Syria

Syria au Siria (Kiar.: سوريا au سورية ) ni nchi ya Mashariki ya Kati au Asia ya Magharibi. Imepakana na Lebanon, Israel, Yordani, Iraq na Uturuki. Kuna pwani ya Mediteranea.

Nchi inatajwa pia kwa jina la "Shamu" katika maandiko ya Kiswahili ingawa neno hili lamaanisha zaidi eneo la kihistoria ambayo ni kubwa zaidi kuliko Syria ya leo.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Wanawake wa Syria, mwaka 1683.

Katika nyakati za kale ilikuwa kitovu cha dola la kwanza la Waarabu na mji mkuu Dameski ulikuwa makao ya makhalifa Wamuawiya.

Kabla ya mwaka 1918 ilikuwa sehemu ya Dola la Uturuki.

Kati ya Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia na uhuru huo ilikuwa nchi lindwa chini ya Ufaransa kwa niaba ya Shirikisho la Mataifa,[2].

Syria ya kisasa imepata kuwa nchi ya kujitawala kwa hatua mbalimbali tangu mwaka 1936 hadi kukamilisha uhuru wake mwaka 1946.[2]

Syria imetawaliwa na chama cha Baath tangu mwaka 1963 na tangu mwaka 2000 rais ni Bashar al-Assad, aliyemrithi baba yake Hafez al-Assad aliyetawala kuanzia mwaka 1970.

Syria ilishiriki katika vita vya Waarabu dhidi ya Israel. Hivyo sehemu ya Mkoa wa Qunaytrah imekaliwa na Israel tangu 1967.

Tangu Machi 2011 nchi imeingia vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyoua watu zaidi ya 100,000 kufikia Septemba 2013.

Mikoa[hariri | hariri chanzo]

Syria kiutawala imegawiwa katikaa mikoa (muhafazat) 14:

Lugha[hariri | hariri chanzo]

Lugha ya kitaifa ni Kiarabu. Kuna pia maeneo penye Wakurdi, Waturuki, Waaramu, Waarmenia na wengineo.

Dini[hariri | hariri chanzo]

Wasyria walio wengi ni Waislamu, hasa Wasunni lakini kuna pia wafuasi wengi kidogo cha aina ya Washia wanaoitwa "Waalawi" n.k. 10% ya wakazi ni Wakristo. Wayahudi wamekuwa wachache sana kutokana na ugomvi kati ya Waarabu na Israel.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Cite error: Invalid <ref> tag; no text was provided for refs named CIA
  2. 2.0 2.1 Report of the Commission Entrusted by the Council with the Study of the Frontier between Syria and Iraq (1932). Iliwekwa mnamo 2013-07-11.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Nchi na maeneo ya Asia

Afghanistan | Armenia2 | Azerbaijan | Bahrain | Bangladesh | Bhutan | Brunei | China | Falme za Kiarabu | Georgia2 | Hong Kong3 | Indonesia | Iran | Iraq | Israel | Japan | Kambodia | Kazakhstan | Korea Kaskazini | Korea Kusini | Kupro2 | Kuwait | Kirgizstan | Laos | Lebanon | Macau3 | Malaysia | Maldivi | Mongolia | Myanmar | Nepal | Omani | Pakistan | Palestina | Qatar | Urusi1 | Saudia | Singapore | Sri Lanka | Syria | Taiwan (Jamhuri ya China) | Tajikistan | Timor ya Mashariki | Ufilipino | Uthai | Uturuki1 | Turkmenistan | Uhindi | Uzbekistan | Vietnam | Yemen | Yordani

1. Nchi ina maeneo katika Asia na Ulaya. 2. Nchi hii iko Asia lakini kwa sababu za kihistoria au kiutamaduni inahesabiwa pia kati ya nchi za Ulaya. 3. Eneo la pekee la China.


BlankAsia.png Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Syria kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.