Nenda kwa yaliyomo

Kugeuka sura

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Yesu Kugeuka Sura)
Mozaiki ya Kugeuka sura, Monasteri ya Mt. Katerina, Mlima Sinai, Misri.
Mchoro mdogo wa Kugeuka sura katika Injili ya Marko, 1300.
Mchoro wa karne ya 12.
Kugeuka sura kadiri ya Lodovico Carracci, 1594: wanaoonekana pamoja na Yesu ni Eliya, Musa na Mitume wa Yesu watatu.
Mchoro wa Alexandr Ivanov, 1824.
Mfululizo wa kurasa juu ya Yesu
Yesu
Yesu Kristo na Ukristo

Umwilisho   Utoto wa Yesu   Ubatizo   Arusi ya Kana   Utume wa Yesu   Mifano ya Yesu   Miujiza ya Yesu   Kugeuka sura   Karamu ya mwisho   Msalaba wa Yesu   Maneno saba   Kifo cha Yesu   Ufufuko wa Yesu   Kupaa mbinguni   Ujio wa pili  Yesu na matabiri ya Agano la Kale   Injili   Majina ya Yesu katika Agano Jipya   Yesu kadiri ya historia   Tarehe za maisha ya Yesu   Kristolojia

Mazingira ya Yesu

Wayahudi   Kiaramu   Bikira Maria   Yosefu (mume wa Maria)   Familia takatifu   Ukoo wa Yesu   Ndugu wa Yesu   Yohane Mbatizaji

Mitazamo juu ya Yesu

Mitazamo katika Agano Jipya  · Mitazamo ya Kikristo   Mitazamo ya Kiyahudi   Mitazamo ya Kiislamu   Yesu katika sanaa

Kanisa la Kugeuka Sura juu ya Mlima Tabor, Israeli, unaohesabiwa na wengi kuwa mahali pa tukio.

Yesu kugeuka sura ni sikukuu ya liturujia ya Ukristo inayoadhimisha fumbo la maisha ya Yesu linalosimuliwa katika Agano Jipya[1], hususan katika Injili Ndugu (Math 17:1–9, Mk 9:2-8, Lk 9:28–36) na katika 2 Pet 1:16–18[1].

Humo tunasoma kwamba Yesu Kristo aliongozana na wanafunzi wake watatu, Mtume Petro, Yakobo Mkubwa na mdogo wake Mtume Yohane, hadi mlima kwa lengo la kusali faraghani.

Huko usiku alianza kung'aa akatokewa na Musa na Eliya waliozungumza naye kuhusu kufariki kwake Yerusalemu.

Kubwa zaidi, Mungu Baba alimshuhudia kuwa Mwana wake mpenzi akawahimiza wanafunzi hao kumsikiliza.[1]

Hivyo Wakristo wanaona tukio hilo kama dhihirisho la Mwana pekee wa Mungu, mpendwa wa Baba wa milele, lililokusudiwa kuonyesha hadi miisho ya dunia kwamba hali duni ya binadamu aliyoitwaa imekombolewa kwa neema na kwamba jinsi ilivyoumbwa kwa mfano wa Mungu, sasa imeumbwa upya katika Kristo baada ya uharibifu uliosababishwa na Adamu [2].

Tukio linaheshimiwa hasa na Ukristo wa Mashariki na wamonaki wanaoliona mwaliko wa kutazama utukufu wa Mungu uliofichama katika malimwengu, kumbe kwa sala unadhihirika kwa macho ya imani.

Fumbo hilo linaadhimishwa kila mwaka kama sikukuu tarehe 6 Agosti[3]. Pia linazingatiwa katika Rozari kama tendo la nne la mwanga.

Marejeo ya Kiswahili

[hariri | hariri chanzo]
  • Masomo ya Breviari - Sikukuu za Bwana, za Bikira Maria na za Watakatifu - Ndanda Mission Press 1978, uk 268-271
  • John Kabeya na wengine - Maisha ya Watakatifu – ed. T.M.P. Book Department – Tabora 1965, 1989, uk. 269-270
  • Pd. Leandry Kimario, O.F.M.Cap. - Mfahamu Mtakatifu Somo Wako - Maisha ya Watakatifu wa Kila Siku pamoja na Watakatifu Wafransisko - Toleo la pili - Dar es Salaam 2021, uk. 229-231
  • Maurice Soseleje, Kalendari yetu – Maisha ya Watakatifu – Toleo la pili – ed. Benedictine Publications Ndanda Peramiho – Peramiho 1986 – ISBN 9976-63-112-X, uk. 62

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  • "The Transfiguration of Our Lord", Butler's Lives of the Saints
  •  "Transfiguration" . Catholic Encyclopedia. New York: Robert Appleton Company. 1913.
  • The Mountain of the Transfiguration Ilihifadhiwa 12 Februari 2012 kwenye Wayback Machine. by Michele Piccirillo
  • Pope Benedict XVI on Transfiguration of Jesus
  • The Holy Transfiguration of our Lord God and Savior Jesus Christ Orthodox icon and synaxarion
Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kugeuka sura kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.