Usiku

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Diunia wa kati wa usiku; picha hii imeunganishwa kutokana na picha mbalimbali zilizopigwa na chomboanga. Hali halisi hakuna wakati ambako eneo lote linaloonekana liko gizani wakati mmoja. Nukta nyeupe upande wa kulia ni nuru ya miji wakati wa giza

Usiku ni kipindi cha siku kilichopo kati ya machweo na macheo na hasahasa kipindi cha giza kinachotokea baada ya macheo ambako mwanga wa jua hauonekani tena angani hadi muda mfupi kabla ya machweo yaani kabla ya jua kuonekana juu ya upeo wa anga. Kinyume chake ni mchana.

Kutokana na kupotea kupotea kwa nuru ya jua nyota zinaonekana usiku (pasipo na mawingu). Watu wengi hulala usiku pamoja na wanyama wengi lakini kuna wanyama wengine wanafanya shughuli zao kwenye usiku kama vile bundi, popo na wadudu wengi.

Nyakati za usiku[hariri | hariri chanzo]

Nyakati za chanzo na mwisho wa usiku hutofautiana kati ya mahali duniani. Mstari unaofikiwa na mwanga wa jua unatembea juu ya uso wa dunia kutokana na mzunguko wa dunia kwenye mhimili wake. Mwendo huu ni sababu ya kugawiwa kwa uso wa dunia katika kanda muda.

Karibu na ikweta muda wa usiku ni masaa 12 sawa na muda wa mchana lakini penginepo duniani mbali ya ikweta kuelekea kaskazini au kusini muda wa usiku hubadilika kila siku.

Usiku mrefu kabisa hutokea kwenye ncha za dunia ambako wala jua wala utusitusi hazionekani angani kwa muda wa karibu miezi 3.

Utamaduni[hariri | hariri chanzo]

Katika tamaduni za binadamu usiku mara nyingi ina maana mbaya kutokana na matatizo ya kuona vema na hofu ya vitu visivyoonekana katika kipindi hiki.

Simple English Wiktionary
Wikamusi ya Kiswahili ina maelezo na tafsiri ya maana ya neno: