Agano Jipya

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Agano Jipya

Agano Jipya ni sehemu ya pili ya Biblia ya Kikristo, ikifuata Agano la Kale: Agano Jipya limefichika katika lile la Kale, na Agano la Kale limedhihirika katika lile Jipya.

Linakusanya vitabu ambavyo Wakristo wote wanaviheshimu kama vitakatifu na vilivyoandikwa baada ya ujio wa Yesu Kristo hadi mwisho wa wakati wa mitume wake.

Vitabu vyake 27 vinaleta habari zake, za mitume wake na za mwanzo wa Kanisa lake.

Vinatakiwa kusomwa kama kilele cha ufunuo wa Mungu kwa binadamu kadiri ya Historia ya Wokovu.

Jina lilitungwa na nabii Yeremia (Yer 31:30) alipotambua kwamba kwa kiasi fulani lile la mlima Sinai lilikuwa na dosari (Eb 8), lakini Mungu kwa uaminifu wake asingeweza kukubali likome tu.

Vitabu vya Agano Jipya ni kama ifuatavyo (Kwa mabano: kifupi cha kawaida kwa kutaja kitabu hiki).

Vitabu vya kihistoria

Injili nne zinasimulia habari za maisha na mafundisho ya Yesu na kutangaza hasa kifo na ufufuko wake.

Kati yake, zile tatu za kwanza zinafanana hata zikaitwa Injili Ndugu, kumbe ile ya Yohane ni ya pekee.

Historia ya mwanzo wa kanisa iko katika mwendelezo ya Injili ya Luka, jina lake

Nyaraka

Nyaraka za Paulo

Kuna maandiko 13 kati ya nyaraka yanayomtaja Mtume Paulo kama mwandishi. Wataalamu wa leo hutofautiana kama kweli nyaraka hizi zote zimeandikwa na Paulo mwenyewe. Kwa jumla saba zimetambuliwa na karibu wataalamu wote kuwa ni maandiko yake. Kuhusu mengine kuna maswali kwa sababu mbalimbali (kwa mfano tofauti za lugha, mkazo tofauti ya mafundisho), na wataalamu wengine hudai ya kuwa labda zimeandikwa na wanafunzi wake au na mwandishi kwa niaba ya Paulo.

Waebrania

  • Waraka kwa Waebrania (Ebr.) una tabia ya pekee; tangu zamani wengine waliulihesabu kuwa waraka wa Paulo ingawa ndani yake jina lake halitajwi. Leo karibu wote wanasema si ya kwake.

Nyaraka katoliki

Jina "katoliki" halimaanisha madhehebu ya Kiroma, lakini maana asilia ya neno la Kigiriki "katoliki" ambayo inaweza kutafsiriwa pia "kwa watu wote".

Kitabu cha kinabii

Kitabu cha mwisho kinafuata mtindo wa kiapokaliptiko, yaani kinatazama historia kwa jumla kadiri ya imani katika ushindi wa Yesu juu ya shetani na nguvu zote za uovu. Kinaitwa

Viungo vya Nje

Toleo la Agano Jipya kwa Kiswahili


ChristianitySymbol.PNG Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Agano Jipya kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.