Waraka wa kwanza kwa Timotheo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Agano Jipya


Barua ya kwanza kwa Timotheo ni kimojawapo kati ya vitabu 27 vya Agano Jipya katika Biblia ya Ukristo.

Pamoja na ile ya pili aliyomuandikia na ile kwa Tito inaunda kundi la Nyaraka za Kichungaji.

Kama vitabu vingine vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa binadamu.

Mazingira[hariri | hariri chanzo]

Barua hii iliandikwa na Mtume Paulo baada ya kifungo chake cha kwanza mjini Roma labda akiwa Makedonia ili kumpa mwanafunzi wake mpenzi mashauri na maelekezo kwa kazi yake aliyomshirikisha.


Kiungo cha nje[hariri | hariri chanzo]

  • [1] Agano Jipya kwa lugha ya Kiswahili