Waraka kwa Wakolosai

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Agano Jipya


Barua kwa Wakolosai ni kati ya vitabu 27 vya Agano Jipya ambalo pamoja na Agano la Kale linaunda Biblia ya Wakristo.

Kama vitabu vingine vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa binadamu.

Muda wa uandishi[hariri | hariri chanzo]

Barua hiyo ni mojawapo kati ya zile za mwishomwisho za Mtume Paulo na inaonyesha maendeleo ya teolojia yake, hasa kutokana na muda mrefu wa kutafakari aliojaliwa kifungoni.

Mazingira[hariri | hariri chanzo]

Kanisa la Kolosai, mji wa biashara karibu na Efeso lilianzishwa na mwanafunzi wa Paulo, labda Epafra, halafu likaingiwa na mafundisho ya ajabuajabu yaliyochanganya mambo ya Kiyahudi na ya Kipagani na yaliyozingatia mno ukuu wa malaika juu ya ulimwengu.

Ndiyo sababu huenda Paulo, akiwa kifungoni Roma kati ya miaka 61 na 63, akawajibika kuliandikia barua inayoonyesha kuwa Yesu Kristo ni mkuu kuliko wote: vyote kabisa viliumbwa kwa njia yake na kwa ajili yake, tena katika ubinadamu wake umo utimilifu wote wa Mungu.

Yeye ndiye “fumbo” kwa kuwa Mungu ametimiza mpango wa wokovu kwa njia yake.

Hakuna sababu ya kutafuta kwingine hekima na maarifa, wala ya kujiwekea masharti ya kibinadamu yasiyosaidia kuokoka (Kol 1:13-29; 2:6-3:4; 3:5-17).

Mpangilio[hariri | hariri chanzo]

Mpangilio wa barua ni kama kawaida ya barua za Paulo: utangulizi, mafundisho ya imani, maonyo kuhusu uzushi, mawaidha na hatima.


Kiungo cha nje[hariri | hariri chanzo]

  • [1] Agano Jipya kwa lugha ya Kiswahili