Epafra

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Epafra.

Epafra (kwa Kigiriki Ἐπαφράς, Epafras) alikuwa mwanafunzi na msaidizi wa Mtume Paulo katika Efeso na mkoa wa Asia.

Inaonekana alikuwa mwenyeji wa Kolosai na alitumwa huko kueneza Ukristo (Kol 1:7; 4;12-13).

Baada ya muda, yalijitokeza huko matatizo ya kiimani yaliyomfanya Paulo aandike barua maarufu kama Waraka kwa Wakolosai.

Paulo anamtaja pia kama mfungwa mwenzake (Waraka kwa Filemoni 1:23).

Kwa jinsi alivyomsifu, tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 19 Julai.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Christian cross.svg Makala hii kuhusu Mkristo huyu bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Epafra kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.