Mtakatifu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

Dini mbalimbali zinaheshimu kwa namna ya pekee watu walio hai au waliokufa ambao walionekana kuwa jirani zaidi na Mungu wakaambukizwa utakatifu wake. Kwa hiyo pengine wanaitwa watakatifu na kutazamwa kama vielelezo vya uadilifu na waombezi.

Katika utamaduni wa Kikristo, watakatifu huchorwa na nembo takatifu, kama ishara ya utakatifu wao; tazama jinsi Yuda Iskarioti (wa mbele kabisa) ni mtume pekee ambaye hana nembo hiyo.

Katika Uyahudi[hariri | hariri chanzo]

Jina linalotumika zaidi ni tzadik (mtu wa haki, mwadilifu), aliyejitahidi kufuata Torati.

Kitabu cha Talmud kinasema kila mara duniani walau 36 tzaddikim wanaishi kati yetu na kuzuia ulimwengu usiangamizwe.

Pengine wanaitwa hivyo hata watu wa mataifa, hasa waliojitahidi kusaidia Wayahudi, k.mf. wakati wa dhuluma.

Katika Ukristo[hariri | hariri chanzo]

Mwanzoni mwa Kanisa kila Mkristo aliitwa mtakatifu kwa sababu alitengwa na ulimwengu na kuwekwa wakfu kwa Mungu aliye mtakatifu, mtakatifu, mtakatifu.

Sifa hiyohiyo ilitolewa pia kwa mahali, siku, vitu n.k. kutokana na matumizi yake ya kidini.

Katika Kanisa Katoliki[hariri | hariri chanzo]

Klara wa Asizi alivyochorwa na Simone Martini katika basilika la Mt. Fransisko wa Asizi huko Asizi

Kwa Wakatoliki mtakatifu ni yule aliyemfuata Yesu Kristo, akiishi kwa upendo na maadili mengine yanayoutegemea, hasa aliyeyatekeleza kwa kiwango cha ushujaa katika kufia dini au katika maisha ya kila siku.

Utakatifu si wa aina moja, bali kila binadamu anatakiwa kuitikia siku kwa siku wito maalumu aliopewa na Mungu. Hivyo yeyote anaweza na kupaswa kulenga utakatifu, bila ya kujali sifa zake za kibinadamu tu.

Ili kuzuia udanganyifu, Kanisa Katoliki linamuachia Papa kusimamia kesi ndefu za kumtangaza mtakatifu mpya, miaka baada ya kifo chake.

Wakatoliki wanawapatia Bikira Maria na watakatifu wengine heshima ya pekee kama marafiki wa Mungu, lakini si ibada halisi. Heshima hiyo inadai wajitahidi pia kufuata mifano yao kama wao walivyofuata ile ya Yesu.

Kwa Waorthodoksi na Waorthodoksi wa Mashariki[hariri | hariri chanzo]

Masalia ya Demetrio wa Thesalonike katika kanisa lake huko Thesalonike

Makanisa ya Kiorthodoksi yanamuita mtakatifu hasa anayesadikiwa yuko katika paradiso, kuanzia Adamu na Eva, Mose na manabii wengine, lakini pia malaika. Ni Mungu anayefunua watakatifu wake kwa kuitikia sala anazotolewa kwa kuwapitia na kwa kutenda miujiza. Wakristo wanaanza kuwatambua lakini uamuzi wa mwisho unachukuliwa na sinodi ya maaskofu.

Waorthodoksi wanawatendea watakatifu kama watu hai, kwa sababu wanaishi mbinguni pamoja na Kristo mfufuka, ingawa miili yao haijaungana tena na roho zao. Kila mtu anapobatizwa anapewa jina la mtakatifu fulani kama msimamizi kwa maisha yake yote.

Katika Uprotestanti[hariri | hariri chanzo]

Madhehebu mengi hayakubali mawazo hayo, yakipenda kusisitiza kwamba wokovu unamtegemea Mungu tu. Hata hivyo mara nyingi waamini bora wanakumbukwa kwa heshima na kuchukuliwa kama mfano (taz. Confessio augustana art. 21). Hasa Waanglikana wanakaribia msimamo wa Wakatoliki na kuadhimisha sikukuu za watakatifu kadiri ya kalenda maalumu.

Katika Uislamu[hariri | hariri chanzo]

Ingawa dini hiyo haikubali tofauti kati ya watu, Waislamu wengi wanapenda kuheshimu kwa namna ya pekee marafiki wa Mungu (wali), wakisadiki wana uwezo wa kutabiri, kuombea na kuponya.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]