Malaika

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
malaika

Malaika katika imani ya dini mbalimbali, kama vile Uyahudi, Ukristo na Uislamu ni kiumbe wa kiroho tu anayeweza kutumwa na Mungu kwa binadamu.

Kwa umbile lake hawezi kujulikana kwa hisi za mwili wetu.

Katika Biblia watatu tu wanatajwa kwa jina: malaika Mikaeli, malaika Gabrieli na malaika Rafaeli.

Katika Uislamu ni kiumbe chepesi ambacho kimeumbwa kwa moto nacho huwa hakanyagi chini kama mwanadamu, bali huelea juu au kuketi ndani ya moyo wa mwanadamu.