Malaika Gabrieli

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Picha ya Gabrieli kwa mtindo wa Kiorthodoksi, 13871395 hivi (Tretyakov Gallery).
Mchoro wa Bikira Maria kupashwa habari na Gabrieli, kazi ya Anton Raphael Mengs.

Gabrieli (kwa Kiebrania גַּבְרִיאֵל|Gavri'el|Gaḇrîʼēl, Mungu ni nguvu yangu; kwa Kiarabu جبريل, Jibrīl au جبرائيل Jibrāʾīl) ni malaika aliyetumwa na Mungu kuleta ujumbe wa pekee katika dini zinazotaka kufuata imani ya Abrahamu.

Kwa sababu hiyo Wakatoliki wanamheshimu kama malaika mkuu pamoja na malaika Mikaeli na malaika Rafaeli, hasa tarehe 29 Septemba[1][2].

Wakristo wengine pia wanamheshimu kwa kupasha habari ya kutungwa kwa Yohane Mbatizaji[3], halafu kwa Yesu[4] inavyosimuliwa na Injili ya Luka.

Waislamu pia wanamheshimu kwa ajili hiyo na kwa kumletea Mtume Muhammad ufunuo wa Kurani.

Kwa mara ya kwanza jina lake liliandikwa katika kitabu cha Danieli.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Martyrologium Romanum
  2. Sikukuu ya Kianglikana huitwa “Michael na Malaika Wote” (kwa Kiingereza Michael and All Angels).
  3. 1:5 Wakati Herode alipokuwa mfalme wa Yudea, kulikuwa na kuhani mmoja jina lake Zakaria, wa kikundi cha Abia. Mke wake alikuwa anaitwa Elisabeti, naye alikuwa wa ukoo wa kuhani Aroni. 6 Wote wawili walikuwa wanyofu mbele ya Mungu, wakiishi kwa kufuata amri na maagizo yote ya Bwana bila lawama. 7 Lakini hawakuwa wamejaliwa watoto kwa vile Elisabeti alikuwa tasa, nao wote wawili walikuwa wazee sana. 8 Siku moja, ilipokuwa zamu yake ya kutoa huduma ya ukuhani mbele ya Mungu, 9 Zakariya alichaguliwa kwa kura, kama ilivyokuwa desturi, kuingia hekaluni ili afukize ubani. 10 Watu, umati mkubwa, walikuwa wamekusanyika nje wanasali wakati huo wa kufukiza ubani. 11 Malaika wa Bwana akamtokea humo ndani, akasimama upande wa kulia wa madhabahu ya kufukizia ubani. 12 Zakariya alipomwona alifadhaika, hofu ikamwingia. 13 Lakini malaika akamwambia, "Zakariya, usiogope, kwa maana sala yako imesikilizwa, na Elisabeti mkeo atakuzalia mtoto wa kiume, nawe utampa jina Yohane. 14 Utakuwa na furaha kubwa na watu wengi watashangilia kwa sababu ya kuzaliwa kwake. 15 Atakuwa mkuu mbele ya Bwana. Hatakunywa divai wala kileo, atajazwa Roho Mtakatifu tangu tumboni mwa mama yake. 16 Atawaelekeza wengi wa watu wa Israeli kwa Bwana Mungu wao. 17 Atamtangulia Bwana akiongozwa na nguvu na roho kama Eliya. Atawapatanisha kina baba na watoto wao; atawafanya wasiotii wawe na fikira za uadilifu, na hivyo amtayarishie Bwana watu wake." 18 Zakariya akamwambia huyo malaika, "Ni kitu gani kitakachonihakikishia jambo hilo? Mimi ni mzee, hali kadhalika na mke wangu." 19 Malaika akamjibu, "Mimi ni Gabrieli, nisimamaye mbele ya Mungu, na nimetumwa niseme nawe, nikuletee hii habari njema. 20 Sikiliza, utakuwa bubu kwa sababu huyasadiki haya maneno yatakayotimia kwa wakati wake. Hutaweza kusema mpaka hayo niliyokuambia yatakapotimia." 21 Wakati huo, wale watu walikuwa wanamngoja Zakariya huku wakishangaa juu ya kukawia kwake Hekaluni. 22 Alipotoka nje, hakuweza kusema nao. Ikawa dhahiri kwao kwamba alikuwa ameona maono Hekaluni. Lakini akawa anawapa ishara kwa mikono, akabaki bubu. 23 Zamu yake ya kuhudumu ilipokwisha, alirudi nyumbani. 24 Baadaye Elisabeti mkewe akapata mimba. Akajificha nyumbani kwa muda wa miezi mitano, akisema: 25 "Hivi ndivyo alivyonitendea Bwana; ameniangalia na kuniondolea aibu niliyokuwa nayo mbele ya watu."
  4. 1:26 Mnamo mwezi wa sita, malaika Gabrieli alitumwa na Mungu aende kwenye mji uitwao Nazareti huko Galilaya, 27 kwa msichana mmoja aitwaye Maria, mchumba wa mtu mmoja jina lake Yosefu, wa ukoo wa Daudi. 28 Malaika akamwendea, akamwambia, "Salamu Maria! Umejaliwa neema nyingi! Bwana yu pamoja nawe." 29 Maria aliposikia maneno hayo alifadhaika sana, akawaza: maneno haya yanamaanisha nini? 30 Malaika akamwambia, "Usiogope Maria, kwa maana Mungu amekujalia neema. 31 Utachukua mimba, utamzaa mtoto wa kiume na utampa jina Yesu. 32 Yeye atakuwa mkuu na ataitwa Mwana wa Mungu Mkuu. Bwana Mungu atampa kiti cha mfalme Daudi, babu yake. 33 Kwa hivyo atautawala ukoo wa Yakobo milele, na ufalme wake hautakuwa na mwisho." 34 Maria akamjibu, "Yatawezekanaje hayo, hali mimi ni bikira?" 35 Malaika akamjibu, "Roho Mtakatifu atakushukia, na uwezo wake Mungu Mkuu utakujia kama kivuli; kwa sababu hiyo, mtoto atakayezaliwa ataitwa Mtakatifu, Mwana wa Mungu. 36 Ujue pia kwamba hata Elisabeti, jamaa yako, naye amepata mimba ingawa ni mzee, na sasa ni mwezi wa sita kwake yeye ambaye watu walimfahamu kuwa tasa. 37 Kwa maana hakuna jambo lisilowezekana kwa Mungu." 38 Maria akasema, "Mimi ni mtumishi wa Bwana, nitendewe kama ulivyosema." Kisha yule malaika akaenda zake.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  • Bamberger, Bernard Jacob, (15 Machi 2006). Fallen Angels: Soldiers of Satan's Realm. Jewish Publication Society of America. ISBN 0-8276-0797-0
  • Briggs, Constance Victoria, 1997. The Encyclopedia of Angels: An A-to-Z Guide with Nearly 4,000 Entries. Plume. ISBN 0-452-27921-6.
  • Bunson, Matthew, (1996). Angels A to Z: A Who's Who of the Heavenly Host. Three Rivers Press. ISBN 0-517-88537-9.
  • Cruz, Joan C. 1999. Angels and Devils. Tan Books & Publishers. ISBN 0-89555-638-3.
  • Davidson, Gustav. A Dictionary of Angels: Including the Fallen Angels. Free Press. ISBN 0-02-907052-X
  • Dennis, Geoffrey. 2007. The Encyclopedia of Jewish Myth, Magic, and Mysticism. Llewellyn LTD.
  • Graham, Billy, 1994. Angels: God's Secret Agents. W Pub Group; Minibook edition. ISBN 0-8499-5074-0
  • Guiley, Rosemary, 1996. Encyclopedia of Angels. ISBN 0-8160-2988-1
  • Kreeft, Peter J. 1995. Angels and Demons: What Do We Really Know About Them? Ignatius Press. ISBN 0-89870-550-9
  • Lewis, James R. (1995). Angels A to Z. Visible Ink Press. ISBN 0-7876-0652-9
  • Melville, Francis, 2001. The Book of Angels: Turn to Your Angels for Guidance, Comfort, and Inspiration. Barron's Educational Series; 1st edition. ISBN 0-7641-5403-6
  • Ronner, John, 1993. Know Your Angels: The Angel Almanac With Biographies of 100 Prominent Angels in Legend & Folklore-And Much More! Mamre Press. ISBN 0-932945-40-6.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu mambo ya dini bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hii kama historia yake au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.