Mwili

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mchoro wa Leonardo da Vinci (1492).
Mchoro wa mwanzo wa karne ya 19.

Mwili ni kile kinachofanya binadamu aonekane na kuishi katika ulimwengu, kwa kufanana na wanyama ambao pia wana mwili.

Tofauti kubwa iliyopo kati ya viumbehai hao, yaani mtu na mnyama, upande wa uwezo wa akili na utendaji pengine inaelezwa na dini, falsafa n.k. kwa kudai uwepo wa roho pia katika umbile la binadamu.

Mwili wa binadamu unaundwa na kiwiliwili pamoja na viungo kwa mfano kichwa, shingo, kifua, mikono mgongo na miguu. Mwili una mifupa 206 ingawa binadamu anapozaliwa huwa na mifupa 270 ambayo baadaye huungana [1].

Umbo lake linategemea urithi lakini pia maisha ya mtu yalivyo. Urefu unategemea mambo mbalimbali, kama vile jinsia, kwa maana kwa kawaida wanaume ni warefu kuliko wanawake.

Kabla ya kufikia utu uzima, mwili unaundwa na seli bilioni 100.000.

Baada ya kufa, mwili wa binadamu unaitwa maiti, wakati ule wa mnyama unaitwa mzoga.

Elimu ya mwili huitwa anatomia.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. How Many Bones Are There In Human Body?.
Makala hii kuhusu mambo ya anatomia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mwili kama matumizi yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.