Nenda kwa yaliyomo

Mwanamke

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Wanawake)
Mama akimnyonyesha mwanae.
Mwanamke mwanabiolojia akimpima kobe wa jangwani kabla hajamuachilia.
Mwanamke akifanya kazi maalumu ya jinsia yake kadiri ya utamaduni wa sehemu nyingi.
Spectral karyotype ya mwanamke.
Mfumo wa viungo vya uzazi wa mwanamke.

Mwanamke ni mwanadamu wa jinsia ya kike, kwa maana anafaa kuwa mke. Ndiyo sababu kwa kawaida anaitwa hivyo aliyefikia utu uzima au walau amebalehe.

Kabla ya hapo huwa anaitwa mtoto wa kike, binti, mwanamwali au msichana.

Baada ya kuzaa anaitwa kwa kawaida mama, jina lenye heshima kubwa katika utamaduni wa aina nyingi.

Akianza kupata wajukuu, anajulikana pia kama bibi.

Wanawake ni takriban nusu ya binadamu wote, wengine huwa wanaume. Ndizo jinsia mbili ambazo zinahesabiwa kwa kawaida kati ya binadamu.

Mwanamke ana tabia zake za pekee upande wa mwili, nafsi na roho, na tofauti kati yao na wanaume hujitokeza kwa namna mbalimbali katika utendaji.

Katika maumbile ya mwili wanawake huwa na viungo vya uzazi vya kike ambavyo ni vya pekee na kulindwa kwa jumla ndani ya mwili.

Msingi wa tofauti hizo ni hasa chembeuzi cha jinsia, yaani wanaume wana jozi la chembeuzi "X" na "Y" ndani ya seli zao zote, lakini wanawake wana jozi la "X" mbili. Chembeuzi Y inabeba habari zote zinazomfanya mwanadamu kukua kama mwanaume badala ya mwanamke.

Lakini si tofauti za mwilini pekee zinazosababisha wanawake kuwa tofauti na wanaume. Kuna pia tabia za kiakili na za kiroho za pekee zinazoonekana wazi kati ya wanawake wengi.

Hata hivyo tofauti nyingi zinategemea pia utamaduni kwa sababu mara nyingi watu wamepanga shughuli na pia namna ya maisha tofauti kwa wanaume na wanawake, hivyo watu wamezoea kuchukua matokeo ya mapatano hayo kama jambo la kimaumbile hata kama ni la kiutamaduni tu.

Pamoja na hayo, kuna wanawake wenye tabia zinazotazamiwa kuwa za kiume. Sababu kuu ni kwamba miili yao huwa na viwango vya homoni tofauti na kawaida. Kuna watu kadhaa wenye mwili wa kike wanaojisikia kuwa wanaume, pengine kutokana na matukio ya utotoni au athari nyingine za kisaikolojia.

Tazama pia

Marejeo

  • Chafe, William H. Ilihifadhiwa 13 Januari 2009 kwenye Wayback Machine., "The American Woman: Her Changing Social, Economic, And Political Roles, 1920–1970", Oxford University Press, 1972. ISBN 0-19-501785-4
  • Roget’s II: The New Thesaurus, (Boston: Houghton Mifflin, 2003 3rd edition) ISBN 0-618-25414-5
  • McWhorter, John. 'The Uses of Ugliness', The New Republic Online, January 31, 2002. Retrieved May 11, 2005 ["bitch" as an affectionate term]
  • McWhorter, John. Authentically Black: Essays for the Black Silent Majority (New York: Gotham, 2003) ISBN 1-59240-001-9 [casual use of "bitch" in ebonics]
  • Routledge international encyclopedia of women, 4 vls., ed. by Cheris Kramarae and Dale Spender, Routledge 2000
  • Women in world history : a biographical encyclopedia, 17 vls., ed. by Anne Commire, Waterford, Conn. [etc.] : Yorkin Publ. [etc.], 1999–2002

Viungo vya nje

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Historia
Dini
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mwanamke kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.