Chembeuzi X



Chembeuzi X (pia: kromosomu X, kutoka Kiingereza X chromosome) ni moja katika jozi ya chembeuzi za jinsia za wanyama wengi kujumuisha mamalia, na kwa hiyo binadamu pia, pamoja na chembeuzi Y. Ndizo zinazosababisha mtu kuwa mwanamume au mwanamke, na vilevile wanyama mbalimbali kuwa wa kiume au wa kike.
Wanawake wana chembeuzi mbili za namna hiyo, ambayo ni chembeuzi XX, na wanaume wana chembeuzi X moja tu pamoja na ile ya Y. Kwa hiyo baba anaweza kumrithisha mwanae akawa mtoto wa kike pindi atakapochangia chembeuzi X kwa mtoto huyo na atamrithisha jinsia ya kiume mtoto pindi atakapochangia chembeuzi Y kwa mtoto huyo. Kwa maana nyingine baba ndiye ambaye anatambulisha jinsia ya mtoto wake.
Chembeuzi X jeni 2,000 hivi kati ya 20,000-25,000 za binadamu, hivyo inabeba jeni nyingi sana kuliko chembeuzi Y. Hivyo kwa mtoto ambaye atakuwa na jinsia ya baba (mume) mara nyingi utaona anabeba na kutokeza sifa za mama, na yule wa kike hutegemea uwezo wa jeni zilizo na nguvu, aidha ni kutoka kwenye chembeuzi kutoka kwa mama au kutoka kwa baba au zikawa na mchanganyiko wa sifa.
![]() |
Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Chembeuzi X kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |