Nenda kwa yaliyomo

Mwanaume

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Mwanamume)
Michelangelo alichonga katika marumaru sanamu ya Daudi kama kielelezo cha umbile la mwanamume.

Mwanaume (vizuri zaidi: mwanamume) ni binadamu wa jinsia ya kiume, kwa maana anafaa kuwa mume. Ndiyo sababu kwa kawaida anaitwa hivyo aliyefikia utu uzima au walau amebalehe.

Kabla ya hapo huwa anaitwa mtoto wa kiume tu au mvulana.

Baada ya kuzaa anaitwa kwa kawaida baba, jina lenye heshima kubwa katika utamaduni wa aina nyingi.

Akianza kupata wajukuu, anajulikana pia kama babu.

Wanaume ni takriban nusu ya binadamu, wengine huwa wanawake. Wanaume na wanawake ni jinsia mbili ambazo zinahesabiwa kwa kawaida kati ya binadamu.

Mwanamume ana tabia zake za pekee upande wa mwili, nafsi na roho, na tofauti kati yao na wanawake hujitokeza kwa namna mbalimbali katika utendaji.

Katika maumbile ya mwili wanaume huwa na viungo vya uzazi vya kiume ambavyo ni pekee kama vile mboo (uume, dhahakari) na mapumbu (korodani).

Wakati wa kubalehe homoni ya testosteroni inaongezeka mwilini mwa mwanaume na kusababisha tabia kama sauti ya chini, kongezeka ya nywele mwilini (kwa mfano ndevu), kuongezeka kwa upana wa mabega na kiwango cha musuli mwilini kulingana na wanawake.

Msingi wa tofauti hizo ni hasa chembeuzi kinachoitwa "Y" yaani wanaume wana jozi la chembeuzi "X" na "Y" ndani ya seli zao zote, lakini wanawake wana jozi la "X" mbili. Chembeuzi Y inabeba habari zote zinazomfanya mwanadamu kukua kama mwanaume badala ya mwanamke.

Lakini si tofauti za mwilini pekee zinazosababisha wanaume kuwa tofauti na wanawake. Kuna pia tabia za kiakili na za kiroho za pekee zinazoonekana kati ya wanaume wengi.

Hata hivyo tofauti nyingi zinategemea pia utamaduni kwa sababu mara nyingi watu wamepanga shughuli na pia namna ya maisha tofauti kwa wanaume na wanawake, hivyo watu wamezoea kuchukua matokeo ya mapatano haya kama jambo la kimaumbile hata kama ni la kiutamaduni tu.

Pamoja na hayo, kuna wanaume wasio wachache sana wenye tabia zinazotazamiwa kuwa za kike kwa sababu miili yao huwa na viwango vya homoni vilivyo tofauti na kawaida. Kuna watu kadhaa wenye mwili wa kiume wanaojisikia kuwa wanawake, pengine kutokana na matukio ya utotoni au athari nyingine za kisaikolojia..

Biolojia na jinsia

[hariri | hariri chanzo]
Alt = Picha ya mtu mzima wa kike, na mwanaume wazima kwa kulinganisha. Kumbuka kuwa mifano miwili imeweka nywele sehemu ya mwili.

Watu wanaonyesha dimorphism ya kijinsia katika sifa nyingi, nyingi ambazo hazina uhusiano wa moja kwa moja na uwezo wa uzazi, ingawa wengi wa sifa hizi zina jukumu katika mvuto wa ngono. Maneno mengi ya dimorphism ya kijinsia katika wanadamu hupatikana kwa urefu, uzito, na muundo wa mwili, ingawa daima kuna mifano ambayo hufuatia muundo wa jumla. Kwa mfano, wanaume huwa na urefu zaidi kuliko wanawake, lakini kuna watu wengi wa jinsia zote ambao wako katikati ya urefu sawa.

Baadhi ya mifano ya tabia za kimwili za kiume za kimwili kwa wanadamu, wale waliopatikana kama wavulana wanawa wanaume au hata baadaye katika maisha, ni:

  • Nywele kuota sehemu za siri
  • Nywele kuota usoni(ndevu)
  • Mabega na kifua kutanuka
  • Fuvu kubwa na muundo wa mfupa
  • Kikubwa cha ubongo na kiasi
  • Misuli kubwa ya misuli
  • Apple maarufu zaidi ya Adam na sauti ya kina
  • Urefu zaidi
  • Tibia ya juu: uwiano wa femar (kiangavu kikubwa kwa kulinganisha na mguu)
  • Andrew Perchuk, Simon Watney, Bell Hooks, The Masculine Masquerade: Masculinity and Representation, MIT Press 1995
  • Pierre Bourdieu, Masculine Domination, Paperback Edition, Stanford University Press 2001
  • Robert W. Connell, Masculinities, Cambridge : Polity Press, 1995
  • Warren Farrell, The Myth of Male Power Berkley Trade, 1993 ISBN 0-425-18144-8
  • Michael Kimmel (ed.), Robert W. Connell (ed.), Jeff Hearn (ed.), Handbook of Studies on Men and Masculinities, Sage Publications 2004

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:


Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mwanaume kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.