Marumaru

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Uchoraji asilia waonekana kwenye uso wa marumaru iliyokatwa na kusuguliwa.
Sanamu ya marumaru yamwonesha mungu wa Kiroma Venus

Marumaru (pia: marmar - kutoka kar. مرمر) ni mwamba wa gange uliobadilika kutokana na joto na shindikizo ndani ya ganda la dunia katika kipindi cha miaka mamilioni. Kikemia ni hasa CaCO3.

Ni jiwe gumu sana inayopatikana katika rangi mbalimbali.

Hupendwa sana kama jiwe la ujenzi hasa kama ni nyeupe. Kama ni haba katika eneo fulani hutumiwa kama mapambo tu yaani kuta zafunikwa kwa marumaru. Jiwe lenye rangi mbalimbali hutumiwa kwa sakafu katika majengo muhimu au kama mapambo ya kuta za ndani.

Tangu kale marumaru ilitumiwa pia kwa sanamu.

Tovuti za Nje[hariri | hariri chanzo]

WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Chem template.svg Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Marumaru kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.