Pambo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Pambo ni zana zinazotumika katika ujenzi na sanaa ya mapambo kutia nakshi eneo au kitu fulani ili kuongeza uzuri wake.

Mapambo kwa ajili ya majengo huchongwa kutoka kwenye mawe, mbao au vito vya thamani, udongo, au pia mengine huchorwa juu yake, k.mf. juu ya kitambaa.

Tangu zamani za kale binadamu ameonyesha kipaji chake cha usanii kwa kupamba vitu mbalimbali, hasa vile vinavyomhusu zaidi, kama vile mavazi yake na mwili wake mwenyewe.

Mitindo mbalimbali ya mapambo imegunduliwa kupitia sanaa na ujenzi, ikiwemo ya ufinyanzi, samani na kazi za uhunzi pia. Kwenye nguo, kuta na vitu vingine ambapo mapambo yaweza kuwa kitu pekee kinachosaidia kuwepo kwake, michoro na miundo pia hutumika zaidi.

Miundo mbalimbali inayotumika katika michoro ya mapambo hutolewa katika maumbo ya kijiometri, na maumbo ya mimea na wanyama pia.

Aina za mapambo anayovalia binadamu[hariri | hariri chanzo]

Makala kuu: Mapambo ya vito

Binadamu, haswa mwanamke, anapenda sana kujitia nakshi kwa mapambo yaliyotengenezwa kwa vito au hata plastiki za rangi. Mapambo hayo ni kama vile:

Herini zinazovaliwa sikioni

Mkufu unaovaliwa shingoni

Kikuba kinachovaliwa nyweleni

Kipini kinachovaliwa puani

Bangili inayovaliwa mkononi

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Blank template.svg Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Pambo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.