Kitenzi
Mifano |
---|
|
Kitenzi ni istilahi ya sarufi kwa maneno yanayotaja matendo kama vile kufanya, kwenda, kulala, kupiga, kuishi na kadhalika.
Lugha nyingi zinatumia vitenzi ingawa kuna pia lugha zisizoweka tofauti kati ya vitenzi na majina.
Maumbo ya kitenzi
[hariri | hariri chanzo]Kwa Kiswahili kila kitenzi kina shina lake linalobeba maana yake. Mfano: ku-fanya ambamo "fanya" ni shina; kiambishi awali "ku-" ni alama ya aina ya neno yaani kitenzi chenyewe.
Ndani ya shina kuna tofauti kati ya mzizi wa neno "fany" na kiambishi tamati ambacho ni silabi "a".
Mzizi wa kitenzi wenyewe haubadiliki wakati wowote kitenzi kinaponyambuliwa katika kauli yoyote iwayo.
Vitenzi kwa Kiswahili hupokea viambishi mbalimbali vinavyoeleza kwa undani zaidi maana ya matumizi ya neno. Viambishi awali ni silabi zilizopo mbele ya mzizi na viambishi tamati ni silabi zilivyopo baada ya mzizi wa kitenzi.
Viambishi awali vinaweza kutaja:
- nafsi ya mtenda - ni nani au nani anayetenda na hivi ni silabi ni /u / a upande wa umoja na tu / m / wa upande wa uwingi mtawalia katika hali yakinishi na "si"/ "hu"/"ha" kuwa vikanushi vya viambishi vya nafsi za mtenda- umoja na "hatu"/"ham"/"hawa" kuwa vikanushi vya viambishi vya nafsi za mtenda-wingi .
- njeo au wakati - kama tendo linatokea sasa au lilitokea wakati uliopita au litatokea wakati ujao ; mifano ni silabi za a pamoja na na kwa wakati wa sasa, li kwa wakati uliopita na ta kwa wakati ujao katika hali yakinishi.
Viambishi tamati vinaweza kupanua au kubadilisha maana ya msingi ya mzizi wa neno. Mifano ni kimbi-a, kimbi-lia, kimbili-ana, kimbi-za, kimbi-zana, kimbi-liwa.
Kwa jumla kitenzi cha Kiswahili kinaweza kuwa na sehemu saba, yaani shina na hadi viambishi sita mbele au nyuma ya shina la neno. Jedwali linalofuata linaonyesha mifano kadhaa. Umbo fupi zaidi ya kitenzi ni amri kama "piga".
1 | 2 | 3 | 4 | 5 | 6 | 7 |
---|---|---|---|---|---|---|
Viambishi awali | Shina | Viambishi tamati | ||||
Viambishi vya Nafsi Mtenda |
Viambishi vya Wakati / Hali |
Viambishi Virejeshi |
Viambishi vya Nafsi Mtendewa |
Viambishi vya Kauli |
Kiishio | |
ni | na | - | - | sem | - | a |
u | me | ni | on | yesh | a | |
a | na | cho | ni | ambi | - | a |
tu | li | po | wa | ingi | z | a |
pig | - | a |
Aina za vitenzi
[hariri | hariri chanzo]- Kitenzi kikuu (T)
- Kitenzi kikuu kisaidizi (TS)
- Kitenzi kishirikishi (t)
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- Vitenzi kwenye "Paneli la Kiswahili" Ilihifadhiwa 3 Desemba 2013 kwenye Wayback Machine.
Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kitenzi kama historia yake, uenezi au maendeleo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |