Mzizi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

Kwa matumizi mengine ya jina hili angalia Mizizi

Mzizi katika isimu ni sehemu muhimu sana ya neno ambayo haibadiliki. Sehemu hii ikibadilika, hata dhana ya neno hilo hubadilika.

Mfano, neno "anakimbia" mzizi wa neno ni "kimbi". Kutokana na mzizi huo, unaweza kuzalisha maneno kama sitakimbia, hakimbii, tunakimbia n.k.

Mzizi wa neno unaweza kuwa wa asili au mnyumbuliko.

Mzizi wa asili ni mzizi ambao hutokana na kitenzi halisi. Yaani, ni mzizi ambao umejengwa kwa shina la neno lililoondolewa irabu "a". Kikanuni tunaweza kusema MZIZI = SHINA - A. Mfano katika neno "anakimbia" shina ni "kimbia". Ili kupata mzizi ni lazima utoe irabu "a", hivyo mzizi utakuwa "kimbi" ambao huo tunaweza kuuita mzizi wa asili.

Kwa upande wa mzizi wa mnyumbuliko, ni mzizi ambao umejengwa kwa mzizi wa asili na viambishi tamati vilivyoondolewa irabu "a". Mfano wa maneno ya mnyumbuliko ni kama vile: chezesha, chezeshwa, chezeka n.k. Mfano kitenzi "Chezesha" mzizi wake wa mnyumbuliko ni "Chezesh", hapo mzizi wa asili ni "Chez" na viambishi tamati ni "esh".

Globe of letters.svg Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mzizi kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.