Nenda kwa yaliyomo

Aina za maneno

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Katika sarufi, aina ya maneno ni kundi la maneno yanayoshiriki sifa zinazofanana za sarufi. Maneno yanayowekwa katika aina moja ya maneno kwa kawaida huonesha mienendo inayofanana ya sintaksia (yaani, huchukua nafasi zinazofanana katika miundo ya kisarufi ya sentensi), wakati mwingine huonesha pia mienendo inayofanana ya mofolojia kwa kuwa hubadilika kwa namna sawa kulingana na hali tofauti, na hata maana zinazofanana kisemantiki.

Aina za maneno zinazojulikana zaidi katika Kiswahili ni: nomino, kitenzi, kivumishi, kielezi, kiwakilishi, kihusishi, kiunganishi, kihisishi.

Istilahi nyingine zinazotumika badala ya aina ya maneno—hasa katika upangaji wa kisasa wa isimu unaojitahidi kufanya utofautishaji wa kina zaidi kuliko ule wa jadi—ni daraja la kisarufi, aina ya kileksika, na kipengele cha kileksika. Waandishi wengine hutumia istilahi kipengele cha kileksika kurejelea tu aina maalum ya kipengele sintaksia; kwao, istilahi hii haijumuishi maneno yanayochukuliwa kuwa maneno ya nasibu, kama vile viwakilishi.

Aina za maneno zinaweza kugawanywa kuwa zilizo wazi au zilizofungwa: aina zilizo wazi (kama vile nomino, vitenzi, na vivumishi) huendelea kupata maneno mapya mara kwa mara, wakati aina zilizofungwa (kama vile viwakilishi na viunganishi) hupata maneno mapya kwa nadra sana, au yasipate kabisa.

Lugha karibu zote duniani huwa na nomino na vitenzi kama aina kuu za maneno, lakini kuanzia hapo kuna tofauti kubwa baina ya lugha mbalimbali. Kwa mfano:

Kutokana na utofauti huu wa idadi ya vipengele na sifa zinazovitambulisha, uchambuzi wa aina za maneno unapaswa kufanywa kwa kila lugha binafsi. Hata hivyo, majina ya kila aina hupewa kwa misingi ya vigezo vya kimataifa vinavyotumika kwa upana.

Aina za maneno

  1. Nomino (alama yake kiisimu ni: 'N')
  2. Viwakilishi (alama yake kiisimu ni: 'W')
  3. Vivumishi (alama yake kiisimu ni: 'V')
  4. Vitenzi (alama yake kiisimu ni: 'T')
  5. Vielezi (alama yake kiisimu ni: 'E')
  6. Viunganishi (alama yake kiisimu ni: 'U')
  7. Vihisishi au Viingizi (alama yake kiisimu ni: 'I')
  8. Vihusishi (alama yake kiisimu ni 'H')

Nomino

Nomino hufanya kazi ya kutaja jina la mtu, kitu au mahali. Kwa mfano: baba, Tanzania, ugonjwa n.k.

Aina za nomino

Kuna aina nne za nomino:

  • 1. nomino za kawaida. Kwa mfano: baba, mama
  • 2. nomino za kipekee. Kwa mfano: Elisha, Angela, Naomi, Christopher
  • 3. nomino za jamii. Kwa mfano: mkutano
  • 4. nomino za dhahania. Kwa mfano: malaika

Viwakilishi

Viwakilishi ufanya kazi ya kusimama badala ya jina au nomino.

Aina za viakilishi

Kuna aina tisa za viwakilishi:

  • 1. viwakilishi vya nafsi. Kwa mfano: mimi
  • 2. viwakilishi vya kuonesha. Kwa mfano: wale
  • 3. viwakilishi vya kumiliki. Kwa mfano: wangu
  • 4. viwakilishi vya idadi. Kwa mfano: wachache
  • 5. viwakilishi vya kuuliza. Kwa mfano: yupi
  • 6. viwakilishi vya kipekee. Kwa mfano: mwenyewe
  • 7. viwakilishi vya a-unganifu. Kwa mfano: la baba
  • 8. viwakilishi vya sifa. Kwa mfano: mfupi
  • 9. viwakilishi vya amba\urejeshi. Kwa mfano: ambalo

Tazama pia

Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Aina za maneno kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.